Staa wa Filamu za Kibongo, Yvonne Sherry ‘Monalisa’.
STAA wa Filamu za Kibongo, Yvonne Sherry ‘Monalisa’ hivi karibuni aliweka wazi kuwa anatamani kuolewa lakini hajampata wa kumuoa.
Monalisa alifunguka maneno hayo baada ya uvumi kuenea kuwa amepata mtu anataka kumuoa na mipango ya ndoa iko tayari.
“Mh! Wewe si wa kwanza kuniambia maneno haya jamani hivi yanatoka wapi? Mimi sijapata mtu wa kunioa jamani ila nikimpata nitaolewa kwa sababu jua limekuchwa pia ndoa ni jambo la heri,” alisema Monalisa.
Katikati ya mwaka huu, Monalisa alionyesha matamanio yake ya ndoa ambapo alivaa shera kwenye harusi ya rafiki yake na kuingia na mumewe ikiwa kama maigizo kituko hicho kiliipendezesha shughuli hiyo.
0 comments:
Post a Comment