Thursday, November 13, 2014

TIMBWILI LA AJABU…MISS NA MUMEWE WAZICHAPA LIVE, SOMA CHANZO HAPA!! *PICHAZ*

MREMBO Mariam Mohamed ambaye alishiriki na kushika nafasi ya pili ya Shindano la Miss Mara mwaka 2003, wiki iliyopita alizusha vurumai kubwa kwa kuzichapa kavukavu na mumewe usiku baada ya kumkuta akiwa na baamed ndani ya nyumba moja iliyopo Njiro eneo linalojulikana kama Nguzo Moja jijini Arusha, Amani lina mkanda kamili.
 
Mrembo Mariam Mohamed akizichapa kavukavu na mumewe, Rasha Idrisa (38).
Licha ya kuzichapa na mumewe huyo ambaye ni mfanyabiashara aitwaye Rasha Idrisa (38), mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam, baamed huyo aitwaye Prisila, naye alipata kipigo kikali toka kwa Miss huyo aliyekuwa akisaidiana kutoa dozi na mpambe wake.
Prissila anayefanya kazi kwenye baa moja iliyopo maeneo ya Njiro (jina linahifadhiwa) alijaribu kujitetea kuwa hakufahamu kama mpenziwe huyo alikuwa mume wa mtu, alishambuliwa sehemu mbalimbali za mwili wake, ikiwa ni pamoja na kukabwa shingo, hali iliyomuacha hoi na kuapa kutoendelea tena kuiba vya watu.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI