Saturday, October 11, 2014

TYLOR SWIFT ATAJWA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2014

MWANAMUZIKI maarufu nchini Marekani Tylor Swift ametajwa kwa mara nyingine kutunukiwa tunzo ya mwanamke bora wa mwaka 2014 na kampuni ya muziki nchini humo ya Billiboard.
Uteuzi huo umemuweka swift kuwa mwanamuziki wa kwanza kupata tunzo ya aina hiyo kwa mara ya pili. 

Tunzo hiyo ambayo hutolewa kwa mwanamuziki wa kike ambae ameonesha ubunifu wa kazi zake na mafanikio kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita imeangukia kwa swift kutokana na mafanikio ya nyimbo zake kufanya vizuri katika chati za muziki za biliboard na kutajwa kuwa mfano wa kuigwa kwa kizazi cha sasa.

Takwimu zinaonesha kuwa, tangu  alipoingia rasmi katika muziki mwaka 2006,  swift ameshaingiza takribani nyimbo 60 katika chati za Billiboard hot  100 hali ambayo haijawahi kutokea kwa mwanamuziki mwingine tangu mwaka huo.

Nyota huyo wa wimbo wa shake it off atapokea tunzo hiyo katika sherehe za utoaji tunzo kwa wanamuziki wa kike  zijulikanazo kama Billiboard Women in Music Award zitakazofanyika mwezi December mwaka huu.


Baadhi ya wanamuziki ambao wameshawahi kupata tunzo hiyo ni pamoja na Pink, Katy perry na Beyonce.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI