Mchezaji mwenye umri mdogo nchini Marekani katika mchezo wa drafti (chess), Sammuel Sevian, huenda akatwaa ubingwa wa juu katika mchezo huo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 13 tayari ameonyesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo huo na tayari ameshaweka historia ya kuwa bingwa katika michezo ya kimataifa iliyofanyika mwaka jana.
Malengo ya Samuel katika mchezo huo ni kuwa bingwa na ana ndoto ya kuwa bingwa mwenye umri mdogo kuiwakilisha Marekani katika mchezo wa drafti.
Licha ya mafanikio hayo Samuel anasema kuwa draft ni mchezo mgumu na kwamba ni vigumu kumwelezea mtu asiyejua kucheza.
Samuel alianza kuonyesha mapenzi na mchezo wa draft akiwa na na umri wa miaka mitano baada ya kufundishwa na baba yake na inaelezwa kuwa ni vigumu kumshauri kufanya jambo lingine mbali na draft.
0 comments:
Post a Comment