Saturday, October 11, 2014

HILI NDILO GARI JIPYA LENYE INJINI MBILI LILILOZINDULIWA NA TESLA

WATENGENEZAJI wakubwa wa magari Tesla, wamezindua gari jipya lenye injini mbili, ambalo limetengenezwa kwa ajili ya kuhimili hali mbaya ya hewa.
 
Mgunduzi wa gari hilo Elon Musk, anasema toleo hilo jipya, litahusisha herufi D ikimaanisha Dual Motor, moja ikiwa sehemu ya mbele na nyingine ikiwa ni sehemu ya nyuma.
Uzinduzi huo umefanyika katika uwanja wa ndege wa Hawthorne Los Angeles nchini Marekani, ambapo ndipo yalipo makazi ya kampuni ya Tesla 
Musk anasema gari hilo, litatolewa katika mifumo mitatu ya 60D, 85D na mfumo mkubwa wa P85D wenye injini yenye nguvu zaidi na kasi yenye uwezo wa kusafiri kilomita 250 kwa saa.

Mfumo wa P85D utatolewa Marekani ya Kaskazini kuanzia mwezi disemba, huku mifumo ya 60D na 85D ikitolewa kuanzia mwezi februari.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI