ULIKUWA ni usiku wa furaha sana kwa staa wa Filamu Bongo, Rose
Ndauka, kwani aliweza kusheherekea siku yake ya kuzaliwa na baadhi ya
mastaa wenzake waliyofurika ndani ya Hoteli ya Collossium iliyopo maeneo
ya Kamata Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Rose
Ndauka (kushoto), akimlisha kipande cha keki rafiki yake mpendwa Jack
Pentzel, muda mfupi baada ya zoezi la kulishana keki kuanza kwenye
sherehe yake ya kuzaliwa iliyofanyika ndani ya
Ukumbi wa Collosseum Hoteli Kamata Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Rose akimlisha keki mwigizaji mwenzake Mayasa Mrisho 'Maya'.
Mwigizaji Jimmy Mafuvu akilishwa keki hiyo na Rose Ndauka.
Maya akifungua shampeni kama ishara ya upendo kwa Rose Ndauka ambaye alikuwa akisherekea siku yake ya kuzaliwa.
Rose Ndauka akimnywesha shampeni Jack Pentzel.
Rose akiselebuka na baadhi ya marafiki zake.
Rose (kulia), akivishwa pete ya dhahabu na dada ake ikiwa kama moja ya zawadi yake katika kusrekea siku ya kuzaliwa kwake.
Jack Pentzel akimmiminia noti Rose Ndauka kama moja ya zawadi yake.
Rose Ndauka akionyesha pete aliyovikwa mkono wa kulia kwake kama moja ya zawadi iliyotoka kwa dada yake.
Mtangazaji wa Times FM, Hadija Sahib 'Dida', akiselebuka na rafiki yake kwenye pati hiyo.
Rose Ndauka akiwa kwenye pozi la pamoja na baadhi ya ndugu na marafiki zake.
Dida akiwa katika pozi na dada yake Rose.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakicheza moja ya muziki uliyokuwa ukipigwa kwenye sherehe hiyo na Rose Ndauka.
Rose Ndauka na baadhi ya wageni waalikwa wakigonga chairs mara baada ya kufungua shampeni iliyokuwa imeandaliwa kwenye sherehe hiyo.
Msanii
nyota wa filamu nchini, Jack wa Chuz akimtunza msanii mwenzake, Rose
Ndauka Sherehe hiyo ya Rose, ambaye alizaliwa siku moja na Rais Jakaya
Mrisho Kikwete, ilishuhudia mastaa wengi wa kike walioalikwa, licha ya
kunywa na kula kwa kadiri walivyojisikia, lakini pia wakiwa wamevalia
vivazi vilivyoonyesha sehemu kubwa ya miili yao.
Katika pati hiyo
kulikuwa na vinywaji vyenye kilevi na visivyo na kilevi, huku pia
vyakula vya aina mbalimbali vikipatikana, kiasi kwamba hadi gazeti hili
linaondoka, pombe na vyakula bado vilikuwepo.
Lakini kivutio zaidi kwenye shughuli hiyo iliyoshuhudia pia Mussa
Issa ‘Cloud’ anayekaimu uongozi wa Bongo Movie Unity akiutangaza upya
umoja wao, alikuwa ni shoga mkubwa wa Rose, Jacqueline Pentezel ‘Jack
Chuzi’ambaye alionekana ‘akimkogesha’ fedha rafikiye wakati wa kutoa
zawadi ulipowadia.
Msanii
nyota wa filamu Bongo, Shamsa Ford naye pia alikuwepo.
Akiwa kwenye
sherehe hiyo, Rose alionekana kuwa mwenye furaha tofauti na siku chache
zilizopita baada ya kukosana na mchumba wake huyo. Katika zoezi la
vinywaji, baadhi ya waalikwa walikunywa hadi kulewa chakari na hivyo
kuleta burudani nyingine.
Baadhi
ya wasanii wa filamu nchini na wageni waalikwa wakila na kunywa. Kwa
upande wake, Rose alisema:
“Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa
kunijaalia afya njema na leo naanza kurejesha furaha yangu na kufungua
ukurasa mpya wa maisha yangu, kwani siku chache zilizopita nilikuwa siko
poa, ila leo nafurahi na ndugu na marafiki zangu kwenye siku yangu
muhimu, najua pati hii imekuwa safi na hakuna aliyeboreka maana mambo
yote yako vyema kabisa.
Picha: GP
0 comments:
Post a Comment