Saturday, October 11, 2014

JAMBAZI SUGU LILILOUA KWA RISASI WANAWAKE JIJINI ARUSHA LAUAWA NA JESHI LA POLISI *PICHA*

picha ya juu na chini  wananchi wa jiji la Arusha  waliojitokeza kuuangalia mwili wa  jambazi huyo hatari aliowawa na polisi usiku wa kuamkia leo
 mwili wa Jambazi hilo ukiwa umelazwa ndani ya gari la polisi mara baada ya kuwawa tayari kwa ajili ya kupelekwa mochwari
 wananchi wakiendelea kushuhudia mwili wa jambazi hilo nje ya jengo la makao makuu ya polisi mkoani Arusha
 baadhi ya vitu vilivyokutwa kwa jambazi hilo zikiwemo silaha mbalimbali
 kamanda wa polisi akionyesha moja ya kifaa cha kufanyia tageti kabla ya kupiga kijulikanacho kwa jina la Glock Fab Defense moja ambacho jambazi hilo lilikuwa likitumia
Jambazi mmoja aliefahamika kwa jina la Ramathan Abdallah  alimaarufu kwa jina la Ramadhani Ndonga (37) mkazi wa  Moivo  ameuwawa baada ya kupigwa risasi katika majibizano na askari  wa jeshi la polisi.

Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas Alisema kuwa tukio hilo limetokea October 10  mwaka huu majira ya saa nane na dakika nne usiku   katika  kijiji cha  Moivo  kilichopo ndani ya kitongoji cha  Enaboishu wilayani Arumeru.

Alisema kuwa marehemu  Ramadhan Abdallh  aliuwa anatafutwa kwa muda mrefu na jeshi la polisi kwa kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu ambayo yameshawahi kutokea ndani ya  mkoa huu pamoja na katika maeneo mbalimbali ya nchi hiii.
Alibainisha  kuwa kuuwawa kwa jambazi hili kumetokana na  juhudi na kutumia mbinu za kisasa za kiupelelezi na kufika  nyumbani kwa mtuhumiwa (marehemu) ambapo askari polisi walimwamuru  ajisalimishe lakini alikaidi amri na kuanza kuwarushia risasi hali ambayo ilisababisha askari kujibu mashambulizi na kumsababishia  umauti kumfika.

“Mara baada yakupiga jambazi huyo polisi walianza kumpekuwa  mwili wa marehemu na alipatiana akiwa ba bastola aina ya Glock 19 yenye namba RLU976 iliotengenezwa nchini Austria ikiwa na magazine yenye risasi (14) ambapo alikuwa ameishika mkononi pamoja na maganda matano yarisasi  na  mbali na hapo polisi pia  walifanya upekuzi katika chumba cha jambazi hilo na kukuta magazine ingine moja yenye risasi (15) na magazine zingine mbili zenye uwezo wa kubeba risasi thelathini kila moja ,Radio call moja  yeye nembo ya ITSS/UNICTR  pamoja na pikipiki aina ya toyo power king rangi nyekundu yenye namba za usajili T507 BSU  pamoja na kofia ngumu”alisema Sabas

Aidha alibainisha kuwa  pia katika upekuzi huo wa ndani ya nyumba ya jambazi hilo pia walifanikiwa kupata pingu moja ,plate namba ingine ya pikipiki yenye namba za usajili T 805 CVD  ambapo alibainisha kuwa jambazi hili lilikuwa likibadilisha plate namba ya pikipiki kila mara  pamoja na  chomba maalumu cha kuwekea magazine pamoja na kufanyia tageti kabla yakupiga risasi (Glock Fab Defense moja),kifaa cha kusafishia bastola pamoja na koti kubwa jeusi.

Kamanda Sabas alitaja baadhi ya matukio ambayo jambazi hili lilishayafanya  kuwa ni pamoja na tukio  lililotekea Augast 6  majira ya saa tatu na nusu usiku maeneo ya kwa iddi ambapo mtuhumiwa  akiwa na mwenzake ambaye ajakamatwa walimpiga risasi ya shingo mwanamke aliyefahamika kwa jina la Shamimu Rashid aliyekuwa mkazi wa sakina wakati akijiandaa kuingina nyumbani kwake  ,huku tukio lingine likiwa limetokea Augast 21 saa 19:00 maeneo ya olasiti ambapo jambazi huyo akiwa na mwenzake kwenye pikipiki walimjeruhi kwa kumpiga risasi ya domo na kutokea kichwani  mototo aitwaye Christen NIckson mwenye umri wa miaka mitatu na nusu na kisha kufanikiwa kumpora TSH 2000 na baadae majeruhi kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.

Kamanda sabas alitumia nafasi hiyo kuwapongeza askari wake kwa kufanya kazi nzuri pamoja na kuwahaidi wananchi kuendelea kufanya uchunguzi na kuwabaini wahalifu wote na kuwachukulia sheria kali.

“arusha sio sehemu ya kuifadhi wahalifu ivyo tutajitaidi kwa hali na mali kuhakikisha tunawamaliza majambazi wote pamoja na wahalifu wote na napenda kuwaaambia wahalifu waache mapema maana sasa ivi tumejipanga vilivyo ,pia napenda kuchukuwa nafasi hii kuwaomba wananchi pia waendelee kuwafichua wahalifu  popote pale ili tuwaangamize kabisa”alisema Sabas

Mmoja wa wananchi ambaye alijitokeza kushuhudia maiti ya jambazi hilo Aliyejitambulisha kwa jina la Alaija Saro akiongea na libeneke blog hili alilipongeza jeshi  la polisi kwa kuweza kumuangamiza jambazi hilo kwani limekuwa likiwatia mashaka watu wengi na kuwanyima raha kwa jinsi walivyokuwa wanauwa watu.
Chanzo: woindeshizza blog

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI