Tuesday, September 23, 2014

HUYU NDIYE MSOMI WA KIISILAMU ALIYELETA KERO HUKO AFRIKA KUSINI! SOMA CHANZO…!

MSOMI wa kiisilamu amefungua rasmi msikiti ambao anasema wapenzi wa jinsia moja wataruhusiwa kusali ndani.Hii ni licha ya kupokea vitisho vya kuuawa na kukosolewa sana na baadhi ya watu wa jamii ya kiisilamu
Wanawake wataruhusiwa kuongoza maombi katika msikiti wa Taj Hargey ambao unaitwa"Open Mosque" mjini Cape Town."tunaunfungua msikiti huu kwa watu wanaowakubali wenzao bila ya kuwabagua,''alisema bwana Hargey. Anasema msikiti huo utaweza kusaidia kukabiliana na itikadi kali za kiisilamu ambazo zinaendelea kukita mizizi katika jamii.
Bwana Hargey, ambaye ni profesa katika chuo cha mafunzo ya kiisilamu mjini Oxford, Uingereza, ameambia BBC kwamba huu ni wakati wa mageuzi ya kidini."miaka 20 iliyopita, Afrika Kusini ilishuhudia mageuzi yaliyofanywa kwa njia ya amani. Kutoka katika enzi ya ubaguzi wa rangi hadi kwa demokrasia na tunahitaji kuwa na hali kama hiyo katika dini, '' alisema bwana Hargey.Hargey aliyefungua msikiti huo anasema hajakwenda kinyume ne dini ya kiisilamu
Amekana kwenda kinyume na mafunzo ya dini ya kiisilamu.Bwana Hargey, mzaliwa wa Cape Town, alisema kuwa watu wa jinsia zote , dini na pia wapenzi wa jinsia moja wanakaribishwa kusali katika msikiti huo.Sawa na kuongoza maombi, wanawake wataruhusiwa kusali katika chumba kimoja na wanaume.
Lengo lake kufanya hivyo anasema ni kumkomboa mwanamke katika dini ya kiisilamu ambaye anasema ameachwa nyuma sana.
Hata hivyo baadhi ya waisilamu tayari wameanza kumkosoa kupitia kwa mitandao ya kijamii wakisema yeye sio muumini.Kikundi kimoja cha vijana kilijaribu kuzuia uzinduzi wa msikiti huo.Viongozi wa kiisilamu wanasema kuwa wanachunguza msikiti huo na pia wameelezea kupata malalamiko kutoka kwa jamii.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI