Wednesday, August 6, 2014

MAMLAKA YA HALI YA HEWA YAWA KIVUTIO KWA WANANCHI KATIKA MAONESHO YA NANENANE MJINI DODOMA

01
Afisa wa Mamlaka ya Hali ya HewaTanzania (TMA) Francis Mariwa akitoa maelezo kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lukundo  juu ya huduma zinazotolewa na mamlaka hiyo wakati walipotembelea katika banda hilo katika  Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kati yanayofanyika katika viwanja vya  Nzuguni mjini Dodoma.Maonesho hayo yamebeba ujumbe wa  “Matokaeo Makubwa sasa” Kilimo ni Biashara.
02
Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Dodoma ambao walifika katika maonesho ya Nanenane wakimsikiliza kwa makini Afisa Uhusiano na Masoko  wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Monica Mutoni  wakatialipokuwa akiwaelezea juu ya shughuli mbalimbali za hari ya hewa  wakati walipotembelea katikabanda lao kwenye maonesho ya Nanenane yanaoyendelea katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma
  03
Akina mama wakazi wa mkaoa wa Dodoma wakimsikiliza kwa makini  Afisa wa Hali ya  Hewa Juma Binda wakati alipokuwa akiwaelezea jinsi wanavyopima  mvua ,wakati walipotembelea banda hilo lililopo katika maonesho ya Nanenane yanayfanyika katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma Maonesho hayo yamebeba ujumbe wa ‘’Matokeo Makubwa sasa “Kilimo ni Biashara.
04 05

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI