Friday, July 18, 2014

JANGA JINGINE MALAYSIA: NDEGE NYINGINE YAANGUKA

NDEGE ya Malaysia, Boeing 777 iliyokuwa inatoka Amsterdam kwenda Kula Lumpur imeanguka Mashariki mwa Ukraine karibu kabisa na mpaka wa Russia, jana July 18. 

Kwa mujibu wa CNN, waziri wa Malaysia anaehusika na mauala ya Usafirishaji amesema kuwa abiria 280 na wafanyakazi 15 waliokuwa kwenye ndege hiyo wamepoteza maisha. 
Maafisa nchini Ukraine wanasema kuwa ndege ya abiria iliyoanguka nchini humo ilidunguliwa katika eneo la mashariki mwa taifa hilo ambako waasi wanaoiunga mkono Urusi wamekuwa wakipigana na vikosi vya serikali. 
Wanasema abiria wote 298 waliokuwa katika ndege hiyo ya shirika la Malaysia iliyokuwa ikisafiri kutoka Amsterdam kuelekea Kualar Lumpur wameufariki. 
Wengi wa abiria hao walikuwa ni raia wa Uholanzi. Rais wa Ukraine Petro Poroshenko alitaja tukio hilo kama kitendo cha ugaidi. 
Maafisa wa Ukraine walichapisha kile walichotaja kuwa mawasiliano ya simu yaliyonaswa kati ya waasi wakiwaeleza maafisa wa Urusi kwamba ni wao ndio waliohusika katika kuindungua ndege hiyo.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Ukraine, Pavlo Klimkin, amesema kuwa serikali ina ushahidi wa kutosha kwamba ndege hiyo ilidunguliwa.
Takriban Abiria 300 wa mataifa mbalimbali wamefariki baada kuanguka kwa ndege hiyo. ' Tulinasa pia mawasiliano ya simu kati ya magaidi hao wakizungumzia kundunguliwa kwa ndege hiyo. Kwa sasa tunatafsiri sauti zao na kisha tutaziweka kwenye mtandao wa internet ili kuthibitisha hilo." 
Hata hivyo sauti hizo zilizonaswa bado hazijathibitishwa na upande uliohuru na waasi hao wamekanusha kuhusika wakisema kuwa ni wanajeshi wa serikali ndio walioidungua ndege hiyo. 
Kadhalika marekani imesema kuwa inaamini ndege hiyo ililipuliwa angani na wala halikuwa tukio la ajali. Makamu wa rais Joe Biden hata hivyo amesisitiza kuwa Marekani bado inatafuta maelezo.
Tukio hili linatokea wakati ambapo bado ndege ya nchi hiyo, Flight 370 iliyopotea March 8 Mwaka huu bado haijapatikana.
Chanzo: BBC

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI