Friday, July 18, 2014

BINTI ALIETUMIA DOLA 30,000 KUFANYA UPASUAJI ILI AFANANE NA KIM KARDASHIAN

Kim kulia na Claire kushoto baada ya kubadili muonekano wake

CLAIRE Leeson Binti wa miaka 24 kutoka London ametumia euro £20,000 (zaidi ya dola 30,000) kufanya plastic surgery ili afanane na Kim Kardashian!
Binti huyo amefunguka kuwa ana kila sababu ya kufanya hivyo kutokana na kuzomewa sana na kuitwa mbaya kipindi yupo shule..
"Nilikuwa naambiwa mimi ni mbaya kuliko kitu chochote kinachoishi na natakiwa nijiue tu..Wakati nimeondoka shule nikaanza kuangalia show ya kina Kim [Keeping Up With the Kardashians] na nikagundua tuna idadi sawa ya ndugu na tuna malumbano sawa ya kifamilia na vitu vinavyoendelea. nikafikiri ni mzuri na nikataka kuwa yeye."

Claire amebadili maziwa yake,akang'arisha meno yake huku akitumia nywele za gharama na anasema anatumaini soon atapunguza mafuta mwilini ambayo yatatumika kwenye makalio yake ili yawe makubwa!
" Nilipopata muonekano wa Kim najisikia najiamini zaidi.. yaani hakuna wa kunigusa wala kunizuia kufanya chochote na naweza kufanya chochote mwenyewe maana nimekuwa najiamini ajabu!."
Kim
Claire

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI