Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernald Membe, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Filamu mpya ya I LOVE MWANZA, ililofanyika mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Membe alilaani vikali wezi wa kazi za wasanii na kutoa Tamko kali dhidi ya Maharamia wanao hujumu kazi za Wasanii.
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kushoto), akizindua filamu mpya iitwayo ‘I Love Mwanza’ iliyoandaliwa na Lake Zone Youth Empowerment Foundation kwa kushirikiana na Tropical Media Tanzania Ltd, katika hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Jumapili Juni 22.2014. Wanaoshuhudia ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba (kulia), Rais wa Bongo Movie, Steven Mengele ‘Steve Nyerere (kushoto) na Mwenyekiti wa Chama cha Sanaa za Maonyesho na Waigizaji Tanzania (TDFAA), Mkoani Mwanza, Anitha Kagemulo (wa pili kushoto).
PICHA NA JOHN BADI
|
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiuhutubia umati wa wananchi waliofurika katika Uwanja wa CCM Kirumba, baada ya kuzindua filamu mpya iitwayo ‘I Love Mwanza’, iliyoandaliwa na Lake Zone Youth Empowerment Foundation kwa kushirikiana na Tropical Media Tanzania Ltd, jijini Mwanza Jumapili Juni 22.2014. |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba (kulia), wakilisakata rhumba lililokuwa likiporomoshwa na Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, katika hafla ya uzinduzi wa filamu mpya ya ‘I love Mwanza’, uliofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Jumapili Juni 22.2014. |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akilakiwa na umati wa wananchi kabla ya kuzindua filamu mpya ya ‘I love Mwanza’, uliofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Jumapili Juni 22.2014. |
Baadhi ya Wasanii wa Jijini Mwanza wakitoa burudani katika uzinduzi huo.
Mahojiano na Waziri baada ya uzinduzi huo.
0 comments:
Post a Comment