Sunday, June 15, 2014

TAARIFA KAMILI KUHUSU MLIPUKO WA BOMU VISIWANI ZANZIBAR, MTU MMOJA APOTEZA MAISHA, WENGI WAJERUHIWA

MTU mmoja ameripotiwa kufariki huku wengine kadhaa wakijeruhiwa katika shambulizi la bomu kisiwani Zanzibar.
Baadhi ya waathiriwa walikuwa wanaondoka katika msikiti mmoja ulioko katika mji mkuu wa Stone Town.
Ni shambulizi la pili la bomu mwaka huu.Haijulikani ni nani aliyetekeleza shambulizi hilo ambalo linajiri mkesha wa sherehe za kimataifa za filamu katika kisiwa hicho.
Mnamo mwezi February, mabomu mawili tofauti ya kujitengezea yalilipuliwa nje ya kanisa Anglikana mjini Stone Town pamoja na mgahawa uliokuwa karibu na kanisa hilo.
Kumekuwa na hali ya wasiwasi wa kidini katika kisiwa hicho.
Chanzo: BBC

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI