Sunday, April 6, 2014

YANGA YAISOGELEA AZAM FC KILELENI, YAINYUKA 5-1 JKT RUVU NA KUFIKISHA POINTI 49, NGASA APIGA HAT-TRICK

Kwa ujumla dakika zote 90 Yanga wametawala zaidi mchezo.

Ngasa amepewa mpira wake baada ya kupiga Hat-trick leo hii
FT: YANGA SC 5 VS 1 JKT RUVU UWANJA WA TAIFA
 Dakika 90` kwa mujibu wa saa yetu zimekatika tunasubiri dakika za mwamuzi
Jeryson Tegete anakosa bao la wazi baada ya kubaki  yeye na kipa wa JKT Ruvu Shaban Dihile
Dakika ya 84 Idd Mbaga anaipatia JKT Ruvu bao la kwanza baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Damas Makwaya
Hassan Dilunga anakwenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Hamis Thabit.
Dakika ya 75` Yanga bado wanaongoza kwa mabao 5-0
Dakika ya 67` Didier Kavumbagu anakwenda benchi, nafasi yake inachukuliwa na Jeryson Tegete
Dakika ya 60` Yanga wanatawala mpira sehemu zote, huku JKT Ruvu wanaoneka kukata tamaa kabisa
Dakika ya 52` Hussein Javu anaifungia Yanga bao la 5, Yanga
JKT Ruvu leo wapo doro kabisa, wanacheza kama wapo mazoezini
Mpira umeshaanza hapa uwanja wa Taifa
Timu zote zinaingia uwanjani tayari kuanza kipindi cha pili
Kwa ujumla katika dakika 45 hizi za kipindi cha kwanza, Yanga wametawala mpira kwa asilimia 60. Wamewadhibiti JKT Ruvu sehemu zote za kiungo na ulinzi, hivyo washambuliaji wao wameshindwa kuonesha makali yao.

 HT: YANGA SC 3 VS 0 JKT RUVU
Dakika ya 45` kipindi cha kwanza Hamisi Kiiza anakwenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Hussein Javu
Wakati wowote mpira unaenda mapumziko uwanja wa Taifa
Dakika ya 49 kipindi cha pili Mrisho Ngasa anaipatia Yanga bao la 4
Dakika ya 40` kipindi cha pili Didier Kavumbagu anaifungia Yanga bao la tatu baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Mrisho Ngasa na mabeki wa JKT walijisahau
Dakika ya 36` Mbuyu Twite aliachia shuti kali na linagonga mtambaa panya
Dakika ya 31` Hamis Kiiza anarejea uwanjani, wakati Kavumbagu anagangwa gangwa. Wakati huo huo Hussein Javu anapasha moto misuli
Dakika ya 30` kipindi cha kwanza, Yanga wanaongoza kwa mabao 2-0
Dakika ya 15` kipindi cha kwanza, Ngasa anaipatia Yanga bao la pili
Dakika ya 8`, Mrisho Ngasa anaipatia Young Africans bao la kwanza.
Dakika ya 6` kipindi cha pili Idd Mbaga wa JKT Ruvu amepiga shuti kali na limegonga mtambaa panya
Dakika ya 5` kipindi cha pili Yanga wanapata kona inayochongwa na Saimon Msuva, lakini mabeki wa JKT Ruvu wanaokoa
Dakika ya 5` kipindi cha kwanza milango bado ni migumu kwa timu zote
Mpira umeshaanza kipindi cha kwanza
.
YANGA SC 0 VS 0 JKT RUVU UWANJA WA TAIFA..
.........................................
Kikosi cha Yanya leo:
1. Deo Munish "Dida" - 30
2. Juma Abdul - 12
3. Oscar Joshua - 4
4. Nadir Haroub "Cannavaro" - 23
5. Mbuyu Twite - 6
6. Frank Domayo - 18
7. Saimon Msuva -27
8. Hassan Dilunga - 26
9. Didier Kavumbagu - 7
10. Mrisho Ngasa - 17
11. Hamisi Kizza - 20
Subs:
1. Barthez, 2. Telela, 3. Job, 4. Zahir, 5. Thabit, 6. Javu, 7. Jerson Tegete

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI