Msanii wa Filamu Tanzania Elizabeth Michael (Lulu) akikumbatiana na Mmoja wa Mashabiki wa Filamu zake katika Eneo la Nyegezi Mwanza Jioni ya jana wakati wasanii wa filamu Tanzania walipotembelea eneo hilo kwa lengo la kutambulisha Shindano la Kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents Mkoani Mwanza, Mahali ni Isamilo Lodge
Baadhi ya Wakazi wa Nyegezi Mwanza wakiwa wamekusanyika kwaajili ya kuwashuhudia wasanii wa filamu Tanzania waliofika katika Viwanja hivyo vya Stendi ya Nyegezi kwaajili ya Kutambulisha Shindano la Kusaka Vipaji vya Kuigiza Tanzania litakaloanzia Jijini Mwanza.
Kijana Mmoja wa Kike ambaye jina lake halikuweza kupatikana haraka akionyesha jinsi ya kushtua Kijoti joti wakati wasanii wa filamu Tanzania Walipofika katika Viwanja vya Stendi ya Nyegezi jioni jana
Msanii wa Vichekesho Joti akimchagua mmoja wa wakazi wa Nyegezi Mwanza kwaajili ya Kupewa zawadi kutoka kwake
Baadhi ya wakazi wa Nyegezi wakinyoosha vidole kwaajili ya kuchaguliwa kujibu swali ambapo mshindi alijishindia Zawadi ya Kopi moja wapo ya Filamu ya Msanii Lulu
Lulu akimkabidhi Zawadi ya Filamu yake ya Foolish Age kijana ambae alipatia kumtaja jina lake halisi wakati wasanii hao walipotembelea viwanja vya Nyegezi Mwanza
Picha ya Pamoja na Mshindi wa zawadi ya Filamu
Msanii Rich Rich akiongea na wakazi wa Nyegezi
Msanii wa Filamu Tanzania Steve Nyerere ambe pia ni Mwenyekiti wa Bongo Movie akiongea na wakazi wa Nyegezi Jioni ya leo wakati wasanii walipotembelea viwanja vya stendi ya nyegezi kwaajili ya Kutambulisha na kuwahamasisha vijana na wazee kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kuonyesha Vipaji vyao Vya kuigiza katika Shindano la Kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents ambalo linaanza rasmi leo jijini Mwanza mahali ni Isamilo Lodge
Wakazi wa Nyegezi Mwanza wakichungulia kwenye gari walilopanda wasanii wa kuigiza Tanzania ambao walifika katika Viwanja vya Stendi ya Nyegezi kwaajili ya kuhamasisha vijana kwa wazee kuweza kujitokeza kwa wingi Hapo leo katika Shindano la Kusaka Vipaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents ambalo litafanyika Isamilo Lodge kuanzia Saa Moja asubuhi na Hakuna Kiingilio.
Picha na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
0 comments:
Post a Comment