Saturday, April 26, 2014

SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MUUNGANO ZAFANA JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete 
akiwapungia mkono wananchi 
waliohudhuria sherehe za miaka 50 
ya Muungano wa Tanganyika 
na Zanzibar zilizofanyika kwenye 
uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam 
na kuhudhuriwa na Viongozi 
mbali mbali wa ndani na nje ya nchi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua 
gwaride la Jeshi la wananchi kwenye sherehe
 za miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.
Kikosi cha Makomandoo kikipita kwa 
mwendo wa aina yake wakati wa sherehe 
za miaka 50 ya Muungano.
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano ambazo zimefanyika katika Uwanja wa Uhuru 
jijini Dar es salaam.
Kikosi cha Makomandoo kikitoa salaam 
kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania katika sherehe za kuadhimisha 
miaka 50 ya Muungano.
Makomandoo wakionyesha namna ya 
kupambana bila kutumia nyenzo hapa 
wakivunja matofali kwa kutumia kichwa 
na mikono.
Baadhi ya silaha zakijeshi zikipitishwa 
mbele ya umati kuonyesha uwezo mkubwa 
wa jeshi letu.
Kikosi cha Wanamaji 
Ndege za kivita zikilinda Ndege ya Rais 
katika maonyesho ya Ndege yaliofanyika 
kwenye Kilele cha Maadhimisho ya miaka
 50 ya Muungano.
Askari wa kikosi cha Mwamvuli akishuka 
kutoka futi 4500 kwenye uwanja wa Uhuru 
kwenye kilele cha miaka 50.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa mkono
 wa pongezi mmoja wa wanajeshi wa 
kikosi cha mwamvuli .
Maandamano ya Pikipiki.
Matembezi maalum ya kusheherekea miaka
 50 ya Muungano .
Njiwa wakirushwa juu kama ishara ya 
miaka 50 ya Muungano ambapo watu 
waliorusha njiwa hao nao wametimiza 
miaka 50.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI