Saturday, April 5, 2014

CHASO IRINGA WATOA TAMKO RASIMU YA KATIBA MPYA

JUMUIYA ya wanafunzi wa Elimu ya Juu Wanachadema Mkoa wa Iringa (CHASO) wamelaani vikali mwenendo mbovu wa Bunge Maalum la Katiba katika kuendesha na kujadili rasimu ya katiba tangu lilipoanza kwa kuendesha malumbano kila kwenye kikao na wakati mwingine wajumbe kuzomeana na kuacha kujadili mambo ya msingi yanayowagharimu Watanzania mamilioni ya Fedha.
Wakitoa msimamo mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za Chaso zilizoko Tumaini katika kata ya Kihesa jana, Katibu Mwenezi wa Chaso Iringa, Michael Noel alisema bunge la katiba limepoteza imani kwa wananchi na wamekuwa wakilipwa posho kwa kodi zetu, wanataka watupatie katiba ya msimamo wa chama cha mapinduzi.
Alisema kuwa chaso haiko tayari kuona mawazo ya wananchi katika rasimu ya katiba yanapotoshwa kwa misingi ya faida ya chama kimoja hivyo wako tayari kuandamana nchini nzima endapo CCM watapitisha katiba yenye msingi ya maslahi ya chama chao.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI