Friday, March 28, 2014

MBUNGE AOMBA BUNGE LA KATIBA LIVUNJWE

MBUNGE Lekule Laiza amemuomba mwenyekiti wa bunge maalum la katiba Mh. Samwel Sitta kumwandikia barua Rais Dkt Jakaya Kikwete barua ya kulivunja bunge hilo kwa kuwa wameshindwa kazi
Mh. Laiza ametoa kauli hiyo leo Machi 27, bungeni wakati akichangia hoja kuhusu upigaji wa kura ya siri ama upigaji wa kura ya wazi, na kusema kuwa wananchi wamekuwa wakiwapigia simu na kuwataka warudi majumbani kwa kuwa wameshindwa kazi
"Kama kazi imetushinda na tunashindwa kufikia muafaka, ni heri mwenyekiti umwandikie rais barua avunje bunge hili, turudi majumbani" amesema Laiza

Amesema kuwa kutokana na bunge hilo kughubikwa na vihoja vya mara kwa mara ni dhahiri kuwa suala hilo limekuwa likiwaumiza vichwa lakini kutokana na umuhimu wa katiba yeye ameshindwa kuona kuwa wao kama wabunge wanafanya nini bungeni, hivyo wanatakiwa kuondoka na kurudi kwao kwa kuwa kazi imewashinda

Kauli hiyo imepingwa vikali na mbunge wa Arumeru mashariki Mh. Joshua Nassari wakati akichangia hoja na kusema kuwa kwa kuwa wamekuja kwa ajili ya katiba, anataka bunge hilo liendelee mpaka kieleweke kilichowaleta yaani kupata katiba mpya kwa kuwa kodi za watanzania zinaendelea kutumika na hivyo inatakiwa waendelee
"nimetoka jimboni kwangu jana tu na ndiyo maana nimeapishwa leo, wananchi wanataka kura ya siri na pia wanataka katiba mpya" alisema Nasari

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI