Friday, March 28, 2014

UHURU KENYATTA AWEKA HISTORIA YA MARAIS WALIOSAFIRI KWA GARI KUTOKA NAIROBI MPAKA ARUSHA

Ni picha ambayo  ikimuonyesha Uhuru Kenyatta ambae ni Rais wa nchi hiyo akiwa na naibu wake William Ruto baada ya kuamua kusimama njiani wakitokea Arusha kwa gari na kula chakula chini ya mti Kajiado.  
(Picha na Rebecca Nduku)
RAIS Uhuru ameripotiwa kufanya mambo kadhaa ambayo hayajawahi kufanywa na Marais wengine wa nchi hiyo likiwemo la kutembea Nairobi bila msafara ambapo hivi juzi kuna video ilitoka ikidaiwa kumuonyesha rais huyo akinunua karanga zilizokuwa zikiuzwa na watoto barabarani Nairobi.
Pichani hapo juu inadaiwa ni msafara wake uliosimama na kula chakula wakati akitokea Arusha Tanzania kwenye mkutano ambapo alitumia usafiri wa gharama nafuu (gari) na kuendeshwa kutoka Nairobi, siku kadhaa tu baada ya nchi hiyo kutangaza kuvunja safari za nje ya nchi za viongozi wa serikali zisizo za lazima ili kuokoa matumizi makubwa ya fedha.
Ni siku kadhaa pia baada ya Rais huyu kutangaza maamuzi ya kupunguza mshahara wake, naibu wake, Mawaziri na hata wakuu wa mashirika ya umma nchini humo.
Picha na Capital fm Kenya.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI