Tuesday, March 25, 2014

LUDEWA WAMPONGEZA RAIS DKT. KIKWETE

WANANCHI wa Ludewa mkoani Njombe wamempongeza Rais Dr Jakaya Kikwete kwa hatua yake ya kuwashirikisha wananchi wa maeneo husika katika suala la utatuzi wa mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi

Hatua ya wananchi hao kumpongeza Rais Dr Kikwete imekuja huku ikiwa ni siku tatu zimepita toka mbunge wao wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe ,mbunge wa jimbo la Kyela Dk. Harrison Mwakyembe na mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi John Komba kurejea nchini kutoka Malawi katika kikao cha usuluhishi wa mgogoro wa mpaka kati ya Malawi na Tanzania

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wananchi hao akiwemo Yohana Haule walisema kuwa hatua ya Rais Kikwete kutumia wananchi wenye kushughulikia suala hilo ni hatua ya kupongezwa kwani wabunge hao ni wawakilishi wa wananchi hivyo kila kinachoendelea kitawafikia mapema wananchi wa maeneo ya mpakani Malawi na Tanzania.

Haule alisema kuwa imani na matumani ya wana Ludewa ni kuona mbunge wao amewawakilisha katika suala hilo na kuwa hawana shaka na uwakilishi wake na wanaamini watapewa mrejesho wa kila kinachoendelea katika suala hilo.

Hivyo alisema kwa sasa hofu ambayo awali wananchi wa kando ya ziwa Nyasa walikuwa nayo juu ya mgogoro huo wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi imeanza kutoweka kutokana na mbunge wao Filikunjombe kuzunguka maeneo yote ya Mwambao na kufanya mikutano na kuwaondoa hofu juu ya hilo.

Huku Sarah Haule mbali ya kumpongeza Rais Kikwete kwa hatua hiyo pia alimpongeza mbunge Filikunjombe kwa jitihada mbali mbali za kuwaletea maendeleo wananchi wa Ludewa huku akimtaka mbunge huyo kuendelea na msimamo wake katika kuwawakilishi wana Ludewa bungeni.
Na Francis Godwin Blog 

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI