MADAKTARI nchini Ujerumani wamewashauri raia kutembea kama ndege aina ya Penguin kwa lengo la kuepuka kuteleza na kuanguka katika kipindi hiki cha baridi jambo linalotokana na kuganda kwa barafu baraabarani.
Madaktari nchini Ujerumani wamewashauri raia watembee kama ndege aina ya penguin katika kipindi hiki cha baridi kali lenye kuandamana na kuanguka kwa theluji ambazo baadae zinaganda na kuwa barafu katika maeneo mengi ya barabara.
Kitengo cha utabiri wa hali ya hewa kimesema hali hiyo itaendelea kwa siku kadhaa na kwamba aina hiyo ya kutembea inayomsadia kiumbe huyo anaeishi katika maeneo ya baridi kali, inaweza kuwanusuru watu na hatari ya kuvunja viungo vyao.
Ushauri huo uliosambazwa kupitia tovuti ya chama cha watoa tiba ya mifupa nchini Ujerumani na ushauri na nasaha unasema kutembea kwa kunyata kunakufanywa na aina ndege huyo, kunaweza kusaidia kukabiliana na kuteleza katika barabara zenye barafu. Lakini kama binadamu atatembea kwa namna yake ya kawaida ni rahisi kuteleza na kuanguka.
Manispaa ya Berlin ilikosolewa vikali mwaka 2014 kwa kushindwa kumwagia chumvi maalumu zenye kusaidia kuyeyusha barafu katika njia nyingi, na hivyo kusababisha idadi kubwa ya watu kuteleza na kuumia.
Timu ya uokozi katika jiji hilo ilipokea simu za dharura 750 na vyumba vyake vya matibabu vilizongwa na idadi kubwa ya watu wenye matatizo ya mifupa. Na kwamba utabiri wa hali ya hewa wa sasa unaonesha kiwango cha joto kitashuka hadi kufikia hadi nyuzi joto -10.
0 comments:
Post a Comment