Saturday, December 17, 2016

MAHAKAMA YA UGANDA YAAMURU KUKAMATWA KWA WIZKID BAADA YA KUSHINDWA KUTOKEA KWENYE SHOW

WIZ KID anakabiliwa na kifungo cha miaka 11 jela, baada ya mahakama ya Uganda kutoa hati ya kukamatwa kwake na meneja wake, Sunday Aare.
Wizkid alishindwa kutokea kwenye show iliyokuwa ifanyike December 3 mwaka huu mjini Kampala. Kampuni iliyomlipa, Face TV, kupitia mwanasheria wake, Fred Muwema, imepata kibali cha kumkamata muimbaji huyo kwa kuchukua dola $60,000 na kushindwa kutokea kwenye show. Gharama zingine walizotoa ni brokerage fee, $5,000 na per die, $3,000 kwa muda ambao Wizkid angekaa Uganda.
Muimbaji huyo alidaiwa kushindwa kusafiri na ndege toka Marekani kwenda nchini humo kwa show hiyo.
“Between 29th August 2016 and 29th November 2016, our client (Face TV) paid to Mr. Sunday Are, Wizkid’s manager the full performance fee of US$60,000, a brokerage fee of US$5,000 and US$3,000 being per diem for the days they were going to stay in Uganda,” yanasomeka maelezo ya mlalamikaji.
Zaidi ya watu 25,000 walikuwa wamenunua tiketi kwaajili ya show hiyo. Maelezo yaliyowasilishwa mahakamani yameeleza kuwa mwandaaji wa shiw hiyo amekula hasara ya zaidi ya $300,000 kutokana na maandalizi aliyofanya.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI