Saturday, October 29, 2016

NYIMBO 5 ZA BONGO FLAVA ZENYE UJUMBE AMBAO SI RAHISI MSANII WA LEO KUUFIKIRIA

Muziki ni sanaa, na sanaa ni ubunifu na upekee. Tasnia ya muziki wa Bongo flava ina miaka zaidi ya 20 sasa na kiukweli tasnia hii imepiga hatua kubwa sana kimaendeleo. Ndani ya kipindi chote hicho cha miaka zaidi ya 20 tumeshuhudia uwepo wa wasanii wengi wenye vipaji maridhawa na nyimbo zenye tija na ubunifu na upekee wa hali ya juu sana ambazo pengine kama wao wasingeimba basi zisingekuwepo kabisa.
Kwa mtazamo wangu, hizi ni nyimbo 5 za Bongo Flava zenye ubunifu usio rahisi kufanyika sasa
ALIKUFA KWA NGOMA – MWANA FA
Ni nyimbo ya pekee, ubunifu na utofauti ni wa hali juu. Meseji ya nyimbo hii ni tofauti sana na nyimbo nyingine zote zenye ujumbe kuhusiana na gonjwa hatari la UKIMWI. Wasanii wengi walioimba kuhusu UKIMWI walionesha kua starehe na uasherati ndio kama chanzo pekee cha gonjwa hili lakini Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’ akasema hapana hata wacha Mungu na wafuasi wa maadili wanaweza kuathirika na gonjwa hili.
NDIYO MZEE NA SIYO MZEE – PROF JAY
Mbunge wa sasa wa jimbo la Mikumi, Mheshimiwa Joseph Haule alikuwa hashikiki enzi zake. Idea za siasa zilikuwa kichwani mwake muda mrefu. Nyimbo hizi mbili ni kama Part One na Part Two. Ndiyo mzee anaomba kura kwa wananchi ambao walimuamini na kumpa uongozi na Siyo Mzee ni kipindi kingine cha uchaguzi ambacho wananchi wanaonesha kumtosa baada ya kutotimiza ahadi zake za awali. Kwa ubunifu huu sioni kama kuna msanii mwingine angeweza kuimba hizi nyimbo kama Profesa Jay asingeimba.
NJE YA BOX - NICK WA PILI
‘Nje ya kumi na nane, nje nje nje ya box, nje ya kumi na nane’ hii ni chorus ya wimbo huu maridadi kabisa wa Hip hop ulioimbwa na kijana wa Hip Hop wa kizazi cha sasa Nick wa Pili akiwashirikisha members wenzake wa Kundi la Weus, kaka yake Joh Makini na G-Nako. 44
Kama ilivyo kwa jina la wimbo hata idea yake kweli ni nje ya box. Kikawaida kwa jamii yetu ya Tanzania na Afrika kwa ujumla wanaume wengi hupenda kuwa wanawake wanaowapenda katika shida na raha na si raha peke yake. Nick aliniacha hoi katika wimbo pale aliomba Mungu amjalie demu mpenda pesa ni kitu cha tofauti sana na ameenda na kinyume na mawazo ya wengi akiwepo Mr Blue aliyeimba ‘nipende kama nilivyo’. Kwa utofauti na ubunifu nisingetegemea kusikia idea hii kutoka kwa mwanamuziki mwingine kama Nick asingeimba.
JUA NA MVUA – JAY MOE
Anajiita Jay Moe Famous. Mimi hupenda kumuita mfalme wa Sinza. Wakati sisi wengine tukichukulia jua na mvua kama mabadiiko ya hali ya hewa tu ambayo ni matokeo ya dunia kulizunguka jua, Juma Mchopanga aliwaza mbali zaidi ya kaamua kuandika wimbo na kutuuliza kipi bora kati ya jua na mvua. Mpangilio wa mashairi ukielezea hasara na faida na kila kimoja kati ya jua na mvua naamini huu ni moja katika ya wimbo wa tofauti sana katika hili game.
MAMA KUMBENA - BANANA ZORRO
‘We mama kumbena, siamini nilichosikia.. Hutaki kumuoza binti, eti kisa umemzoea..’ haha it’s funny, inachekesha sana lakini Banana Zorro alifanya huu utunzi. Kwa jamii zetu za kiAfrika mtoto wa kike kupata mume wa kumuoa ni neema sana lakini mama Kumbena alimnyima mke Banana Zorro eti kisa amemzoea Kumbena. Siju kama ni true story au ni utunzi lakini ubunifu huu na utofauti ni ngumu kidogo kwa msanii mwingine kupata concept kama hii.
NYINGINEZO
Nyimbo zingine kwa haraka haraka ambazo naona utofauti na mawazo tofauti ambayo si rahisi kwa wasanii wengine kuimba endapo wasingeimba walioimba nyimbo hizo ni kama Usiniseme ya Alikiba, Pii Pii Ya Marlaw na Bado Nipo Nipo ya Mwana FA.
#Na Javan Watson

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI