Kwa sasa inaweza kuthibitishwa rasmi na kwa usahihi kuwa ratiba ya kumpatia heshima za mwisho kumuaga kiongozi wetu mahiri na kipenzi cha watu Alphonce Mawazo imebadilika.
Baada ya mashauriano kupitia vikao yaliyofanyika takriban siku nzima ya jana hadi usiku, imekubalika kuwa Mawazo hatazikwa kesho Jumatatu kama ilivyokuwa imepangwa awali na leo hataagwa mjini Geita kama ambavyo wananchi walikuwa wameshataarifiwa kupitia njia mbalimbali.
Taarifa ya ratiba nyingine kuhusu utoaji heshima za mwisho kumuaga Mawazo na mazishi yake, itatolewa baadaye.
Asanteni
Tumaini Makene
0 comments:
Post a Comment