Mgombea
Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,
akihutubia mkutano wa kampeni katika viwanja vya Kandwi jimbo la Chaani
Unguja.
Wafuasi wa CUF wakimsikiliza mgombea wao wa Urais katika viwanja vya Kandwi jimbo la Chaani.
Wafuasi wa CUF wakimsikiliza mgombea wao wa Urais katika viwanja vya Kandwi jimbo la Chaani. (Picha na OMKR).
Na:Hassan Hamad (OMKR)
Chama Cha Wananchi CUF kimewahakikishia wakulima wa mwani bei nzuri ya zao hilo iwapo wananchi watakipa ridhaa ya kuingia madarakani katika uchaguzi mkuu ujao.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Chama hicho Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameeleza hayo wakati akiwahutubia wafuasi wa chama hicho katika mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Kandwi jimbo la Chaani.
Amesema kwa muda mrefu wakulima wa mwani wamekuwa wakiishi maisha duni kutoka bei ndogo ya kilimo hicho ikilinganishwa na gharama za uzalishaji, jambo serikali yake italipa umuhimu wa kipekee.
Amesema kama ilivyo kwa zao la karafuu, serikali atakayoiongoza itafanya utafiti wa bei ya mwani duniani, ili wakulima ambao wengi wao ni wanawake, waweze kunufaika ipasavyo na kilimo hicho. Sambamba na hilo Maalim Seif amesema iwapo atachaguliwa serikali yake itafanya utaratibu wa kulisarifu zao hilo hapahapa nchini, ili kuliongezea thamani yake katika soko.
Aidha Maalim Seif amesema anakusudia kufanya mapinduzi ya kijani kwa kuwawezesha wakulima kulima mazao mengi zaidi yenye tija, na mapinduzi ya buluu kwa kuwawezesha wavuvi kuvua katika bahari kuu.
“Tutawatoa wakulima kutumia jembe la mkono na kuendeleza kilimo cha kisasa”, alisisitiza. Amesema pia wakulima watapatiwa utaalamu kuweza kulima mazao ya viungo yakiwemo tangawizi, ili kuepuka kuagizia mazao hayo Tanzania bara. Katika hatua nyengine mgombea huyo wa urais kupitia CUF amesema ataweka utawala wa sheria ili kila mtu aweze kupatiwa haki yake kwa mujibu wa sheria zilizopo.
“Hakuna atakayeonewa, kila mmoja atatendewa haki sawa sawa na mwengine, na wala hakuna atakayekuwa juu ya sheria”, alieleza.
Kuhusu vitendo vya rushwa ameahidi kupambana na vitendo hivyo kwa nguvu zake zote, kuweka maslahi mazuri kwa wafanyakazi, ili Zanzibar iweze kuendelea bila ya rushwa, na kwamba rushwa imekuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo.
Amefahamisha kuwa sheria zinazohusiana na rushwa zitapitiwa upya kuwezesha wanaojihusisha na vitendo hivyo kuchukuliwa hatua bila ya muhali au kuoneana haya.
Katika salamu zake kwa wanawake wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mwakilishi wa viti maalum anayemaliza muda wake kutoka Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Mhe. Kazija Kona, amewataka wanawake wa Mkoa huo kumchagua Maalim Seif, ili waondokane na kero ya kuwalipia ada nyingi watoto wao maskulini.
Ameeleza kuwa serikali ya inayoongozwa na CCM iliwaahidi wananchi kuwapatia elimu bora bila ya malipo, lakini wazazi wamekuwa wakibeba mzigo mzito wa kulipia ada watoto wao, licha ya maisha magumu yanayowakabili.

#Michuzijr
0 comments:
Post a Comment