KWA wale walioshiba siku wanaweza kabisa kukumbuka filamu ya mwaka 1973 ya Enter the Dragon na ile ya Black belt Jones ya mwaka 1974.
Filamu hizo ni kati ya filamu lukuki ambazo zilimtambulisha james Milton aka Jim Kelly.
Muigizaji huyu wa Marekani ambaye alizaliwa Mei 5,1946 alifariki dunia Juni 29,2013 alikuwa mpiganaji wa kweli wa karate na alitumika vyema katika miaka ya 1970 , miaka ambayo waigizaji wa Kiafrika wa Marekani na wadhamini waio walikuwa wanapambana kutoka na kujenga heshima ya uafrika.
Kelly ambaye alizaliwa Millersburg, Kelly alianza masuala ya sanaa na burudani akiwa katika shule ya Bourbon County High School iliyopo Paris, Kentucky na akawa anashiriki kiushindano katika michezo ya kikapu, mpira wa miguu na riadha.
Msanii huyu pia alipitia katika Chuo Kikuu cha Louisville lakini hakumaliza na kuamua kwenda kujifunza mapifanio ya kujihami ya Karate mfumo wa Shorin-ryu.
Alijifunza chini ya mwalimu Sin Kwan The (Shaolin-Do) mjini Lexington, Kentucky.
Pia alijifunza miondoko ya Okinawan chini ya Parker Shelton, Nate Patton, na Gordon Doversola.
Katika miaka ya 1970 kelly akawa mtu maarufu sana katika mashindano ya karate.
Mwaka 1971, Kelly alitwaa makombe manne ya mchezo huo katika kipindi cha mwaka mmoja. Katika mwaka huo alitwaa ubingwa wa dunia uzito wa kati katika karate.
Baadae alifungua shule yake mwenyewe (dojo) ambayo ilikuw ainatembelewa kila mara na mastaa mbalimbali wa Hollywood. Pia alimfundisha karate muigizaji Calvin Lockhart. Mafunzo hayo yalilenga kumweka sawa na uigizaji wake katika sinema ya Melinda ya mwaka 1972 na pia kuigiza kama mwalimu wa mapigano ya kujihami.
Pamoja na uigizaji na uchezaji karate,Kelly pia alikuwa ni mcheza tenisi wa kulipwa na kabla yake alicheza tenisi ya kawaida.
Kama muigizaji , Kelly alikuwa mwafrika wa kwanza kucheza filamu za Kung Fu . Aliigiza na Bruce Lee katika filamu lililofanya vyema la Enter the Dragon (1973) katika nafasi ambayo awali ilipangwa kuchexzwa na Rockene Tarkington ambaye aliachia ngazi hiyo muda mfupi kabla ya kuanza kuigizwa kwa sinema hiyo mjini Hong Kong.
Inasemekana projuza Fred Weintraub alishasikia mambo ya Kelly na kwenda katika ofisi zake kumuona na kumpenda na kuamua kuingia mkataba naye.
Nyingi ya filamu za Kelly ni zile ambazo zilimuonesha kwamba ni mwafrika mwamerika anayefua watu mafunzo ya karate,.
Mkali huyu alipata nafasi ya kuigiza filamu tatu baadae baada ya kumaliza sinema ya Enter the Dragon na Melinda.
Warner Brothers walimchezesha katika Three the hard way (1974) akiwa na akina Jim Brown na Fred Williamson na Hot Potato mwaka 1976 na ya kumuokoa mtoto wa mwanadiplomasia katika misitu Thailand.
Baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa sinema tatu na Warner Brothers, alicheza katika sinema za Black Samurai (1977) Death Dimension (1978) na Tattoo Connection (1978).
Baada ya kuigiza katika sinema ya One Down, Two To Go (1982) Kelly akawa nadra sana kuonekana katika filamu hadi alipotokea kwa jamu katika Undercover Brother (2002) akiwa na Eddie Griffin na picha yake ya mwisho ilikuwa Afro Ninja (2009) akiwa kama Cleavon Washington .
Mwafrika huyu mwenye historia kidogo lakini picha zenye aksheni babu kubwa alifariki dunia Juni 29,2013 nyumbani kwake san Diego, California akiwa na umri wa miaka 67 kw augonjwa wa kansa.
Filamu alizocheza na nafasi:
• Melinda (1972) kama Charles Atkins
• Enter the Dragon (1973) kama Williams
• Black Belt Jones (1974) kama Black Belt Jones
• Three the Hard Way (1974) kama Mister Keyes
• Golden Needles (1974) kama Jeff
• Take a Hard Ride (1975) kama Kashtok
• Hot Potato (1976) kama Jones
• Black Samurai (1977) kama Robert Sand
• The Tattoo Connection (a.k.a. E yu tou hei sha xing, Black Belt Jones 2) (1978) kama Jones
• Death Dimension (1978) kama Lt. Detective J. Ash
• The Amazing Mr. No Legs (a.k.a. Mr. No Legs) (1979)
• One Down, Two To Go (1982) kama Chuck
• Stranglehold (1994)
• Ultimatum (1994) kama Executive
• Macked, Hammered, Slaughtered and Shafted (2004) kama Executive
• Afro Ninja (2009) kama Cleavon Washington
Na kwenye televisheni
• Highway To Heaven (1985/1986) (2 episodes) kama Ripota
•
Source:Na Oliva Kibua
0 comments:
Post a Comment