Monday, August 31, 2015

UKAWA YAMTANGAZA RASMI JULIUS MTATIRO MGOMBEA WA JIMBO LA SEGEREA

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea kupitia CUF, Julius Mtatiro.
Ndugu zangu, hivi punde nimepokea simu za Hongera kutoka kwa waandishi kadhaa wa habari waliotoka kwenye mkutano wa UKAWA wa kutangaza majimbo ambayo yalikuwa hayajagawanywa. Wamenijulisha kuwa jimbo la Segerea limewekwa chini ya CUF katika nafasi ya ubunge ikiwa na maana kuwa nakuwa mwakilishi rasmi wa UKAWA katika jimbo hili.
Nimeongea na viongozi wakuu wa vyama ambao wamenithinitishia taarifa hizi na kwa hivyo naziweka hapa kama taarifa rasmi.
Nitumie fursa hii kuwashukuru wana Segerea wote ambao kwa wiki kadhaa simu zao hazikuisha kuja kwangu, wote niliwataka tusubiri maamuzi yafanywe na sasa yameshatangazwa rasmi na tutaendelea na kazi iliyobakia, kuliletea taifa mbunge wa UKAWA kutoka hapa Segerea.
Jambo moja ambalo nataka niwaahidi wanachama wa CUF na CHADEMA ni kwamba natambua mgawanyo wa kata zote 13 ulishafanywa na viongozi wa wilaya na majimbo wa vyama vyetu.
Nitasimamia utekelezaji huo na nitawanadi na kuwapigania madiwani wote wa UKAWA. Chama changu kimepewa kata 5 na CHADEMA ina kata 8, kama kuna kata yoyote imeingiliwa na diwani asiyehusika tutahakikisha anajitoa kabla ya kuisha wiki hii ili 25 Oktoba niwakabidhi madiwani 13 waliochaguliwa na wananchi.
Namshukuru sana dada Anatropia Theonest kwa kusubiri maamuzi haya kama mimi. Natambua mchango wake katika kuimarisha upinzani Segerea na namuomba aungane nami tusimamie mabadiliko haya muhimu.

Nawaomba wananchi wote wa Segerea wenye kata zote 13 wajipange kwa nguvu zote. Tangazo la uzinduzi wa kampeni za UKAWA litatoka Kesho usiku mara baada ya kikao cha viongozi wote.
Marafiki na wananchi wa ndani na nje ya Segerea, ndani na nje ya Dar Es Salaam wanaweza kushiriki nasi katika safari hii ya ukombozi kwa kutuchangia kupitia akaunti za simu, kiasi chochote kile cha fedha:
MPESA 0755 855 144,
TIGOPESA 0717 536 759,
AIRTEL MONEY 0787 536 759.
Ni mimi,
Julius Mtatiro,
Mbunge Mtarajiwa wa Jimbo la Segerea,
Whatsup 0787536759,

juliusmtatiro@yahoo.com

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI