JAMAA mmoja alijiandalia mazingira poa
kabisa ya kuzamia kwenye ndege toka Ethiopia mpaka Sweden… alifika
salama lakini hiyo bahati ya kuingia mitaa ya Sweden na kuanza maisha
haikuwa upande wake, alinaswa mapema mapema baada ya ndege kutua Uwanja
wa Ndege Arlanda, uliopo Sweden.
Jamaa alikamatwa na kukabidhiwa mikononi
mwa Askari, alikutwa akiwa amejificha kwenye sehemu ya kuweka mizigo
kwenye ndege hiyo ya Ethiopia Airlines, japo sehemu
hiyo inakuwa na baridi kali sana lakini wakati ndege ikiwa safarini
lakini kinachoshangaza ni kwamba jamaa kakutwa yuko sawa kabisa hana
tatizo lolote kiafya.
“Wafanyakazi walipokuwa wanashusha mizigo walimkuta huyo mtu, yuko sawa kabisa ila tumemkabidhi wakamcheki afya yake pia”—hiki ndio alichokisema Henrik Klefve, Msemaji wa Kampuni ya Swedavia inayosimamia shughuli za Uwanja huo wa Ndege.
Ofisa wa Polisi Anders Faerdigs amesema haya pia kuhusu mtu huyo >>>>
“Amesema
alikuwa anafanya kazi Uwanja wa Ndege Addis Ababa, na tumemkuta na
kitambulisho chake pia.. ndio maana aliweza kuingia na kujificha ndani
ya ndege kirahisi”
Kingine ni kwamba wanahisi alijificha
sehemu ya mizigo ambako huwa wanasafirishwa wanyama ambako kidogo kuna
joto la kawaida kuliko sehemu ya mizigo ambayo ina baridi kali sana.
0 comments:
Post a Comment