Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya kuratibu
Harambee ya kuwachangia waandishi wa habari wanaougua maradhi mbalimbali
ikiwemo ugonjwa sugu wa saratani Bw. Benjamin Thompson Kasenyenda akitoa wito
kwa watanzania wote wenye mapenzi mema kujitokeza kwa wingi kushiriki katika
harambee hiyo itakayofanyika katika viwanja vya Leaders club,siku ya Jumamosi
Julai 4,2015 wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam.kushoto
ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene.Kulia ni wajumbe
wa Kamati hiyo Bi. Mwanamkasi Jumbe na Angela Msangi.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah
Mwambene akiwahamasisha waandishi wa habari kuimarisha mshikamano katika
Harambee ya kuwachangia waandishi wa habari wanaosumbuliwa na magonjwa sugu
ikiwemo kansa.Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo Bi. Grace Nakson
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi
Kawawa ambaye ni mjumbe wa kamati ya kuratibu Harambee ya kuwachangia
wanahabari wanasumbuliwa na magonjwa sugu ikiwemo kansa akiwahamasisha wanahabari wote nchini
kuungana katika harambee hiyo kwa kuihamasisha jamaii kushiriki katika tukio
hilo muhimu. Kushoto ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Maandalizi ya kuratibu Harambee ya kuwachangia waandishi wa habari
wanaougua maradhi mbalimbali ikiwemo
ugonjwa sugu wa saratani Bw. Benjamin Thompson.
Bw. Robert Latonga kutoka TV 1 (Wa kwanza aliyeshika kamera) na Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa
kuhamasisha kuwachangia waandishi wa habari wanaougua maradhi mbalimbali
ikiwemo ugonjwa sugu wa saratani.
Mjumbe wa Kamati ya Kamati ya Maandalizi ya kuratibu
Harambee ya kuwachangia waandishi wa habari wanaougua maradhi mbalimbali
ikiwemo ugonjwa sugu wa saratani Bi.
Angela Msangi akiwahamasisha wanahabari kujitokeza kwa wingi katika harambee
hiyo na pia kutumia taaluma yao kuihamasisha jamii kujitolea katika kufanikisha
lengo la harambee hiyo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo Bi. Mwanamkasi Jumbe.
0 comments:
Post a Comment