Mjumbe
wa Bodi ya Filamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bi.Vicensia
Shule(wa kwanza kutoka kushoto) akimwuliza jambo Mwenyekiti wa
makampuni ya Proin Bw,Johnson Lukaza(hayupo pichani) leo jijini Dar es
salaam walipotembelea kujionea miundombinu ya kampuni hiyo.Kutoka kulia
ni Makamu mwenyekiti wa wa Bodi iyo Bw.Sylvester Sengerema na katikati
ni Bw.Bishop Hiluka.
Mtendaji
Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo akichangia jambo wakati
walipotembelea miundombinu ya Filamu ya Makampuni ya Proin.Bi Fissoo
ametoa wito kwa makampuni yanayotengeneza Filamu Tanzania kuendelea
kushirikiana na Serikali ili kuimarisha Tasnia ya Filamu na
kusaidia katika kupambana na Changamoto mbalimbali.
Mwenyekiti
wa Makampuni ya Proin Bw. Johnson Lukaza akimwonyesha Katibu mtendaji
wa Bodi ya Filamu Bi,Joyce Fissoo moja ya Kazi walizotengeneza na
kuingia Sokoni,Pia aliiomba Serikali kusaidia kuweka sheria kali
zitakazo zuia wizi wa Filamu nchini.
Wajumbe wa Bodi ya Filamu Tanzania wakifurahia jambo na Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin Bw,Johnson Lukaza(wa tatu kutoka kushoto) walipotembelea miundombinu ya kutengenezea filamu ya Kampuni iyo eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam.Wajumbe hao walijionea jinsi Filamu inavyotengenezwa na pia walitembelea eneo kampuni iyo wanapojenga Studio ya kutengenezea Filamu.
0 comments:
Post a Comment