Wednesday, June 10, 2015

MZENJI MPYA YANGA TISHIO SIMBA

KIUNGO wa Simba, Awadh Juma, ametamka kuwa kitendo cha Yanga kupata sahihi ya beki wa kushoto, Mwinyi Ngwali ni tatizo Msimbazi kwani mchezaji huyo yuko kwenye ubora na hanaga masihara kazini.

Awadh amesema uwepo wa Ngwali aliyesajiliwa kutoka KMKM ya Zanzibar utaimarisha safu ya ulinzi ya Yanga kutokana na staili yake ya uchezaji na hata katika mchezo watakaokutana, inawabidi wawe waangalifu na mtu huyo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Awadh alisema: “Timu zimefanya usajili kutokana na mahitaji yao, lakini usajili wa Yanga kwa beki yule wa kushoto Ngwali, wamepiga bao sana kwani jamaa anajua.

“Namjua vizuri, pia tumeshacheza pamoja Zanzibar Heroes, ni beki ambaye anajitambua na anatumia akili, ana uwezo wa kupiga mipira mirefu, anapanda na anakaba.

Kutokana na hali hiyo, Yanga itakuwa vizuri sana kwa upande huo.”

Usajili wa Ngwali Yanga unaelezwa kwamba ni mapendekezo ya nahodha, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kuwa mchezaji huyo ni jembe. Cannavaro pia amehusika kwenye usajili wa Malimi Busungu wa Mgambo Shooting.

Mpaka sasa, Yanga imewasajili Ngwali, mlinda mlango, Benedict Tinocco, mawinga Deus Kaseke, Malimi Busungu na Geofrey Mwashiuya.


Simba nayo imeshawasajili, mlinda mlango wa JKU Mohammed Abraham, winga Peter Mwalyanzi kutoka Mbeya City, Haji Nuhu aliyeichezea Azam FC hapo nyumba na Fakhi Mohammed kutoka JKT Ruvu.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI