Mwimbaji Injili Bongo, Rose Muhando.
***********
ROSE Muhando, aliye
mwimbaji Injili Bongo, amejikuta akimwaga machozi yaliyojaa uchungu huku
akitumia kama dakika 45 kuelezea wazi mateso na manyanyaso ambayo
anayapitia kwa sasa ikiwemo kuhusishwa na tuhuma za utapeli na ‘kubwia
unga’, Risasi Jumamosi linakupa stori kamili!
ILIKUAJE?
Mwandishi wetu
alimtafuta mwimbaji huyo juzi kwa njia ya simu kutoka mkoani Dodoma
yaliko makazi yake lengo likiwa kujua maendeleo yake kikazi ndipo
kukaibuka mapya mengi.Rose alianza kuporomosha lawama dhidi ya watu
wanaomzushia mambo yasiyo ya kweli juu yake:
MSIKIE MWENYEWE
“Aah, mimi nipo tu
(Dodoma) nimekaa kimya kwa sababu si mtu wa majibizano na malumbano,
nimepakwa uchafu wa kila aina na kutukanwa huku wanaonitukana ni
Wakristo wenzangu na mbaya zaidi hadi wachungaji wananisakama kwa maneno
makali, nikaona kukaa kimya ni hekima.”
TUENDELEE
Rose alisema, alichukua
uamuzi wa kuachana na dini yake ya zamani (Uislamu) na kujiunga na
Ukristo kutokana na kuguswa na mafundisho yake baada ya kuhubiriwa
upendo wa kweli lakini kwa sasa anakutana na maumivu na kusalitiwa huku
wakisahau mema anayofanya kwa kutangaza Injili.
HUYU HAPA TENA!
“Wakristo wamenifundisha
ugaidi na ukatili, ndugu zangu ni Waislamu, kila siku hawaachi kunisuta
kutokana na matusi ninayotukanwa na Wakristo wenzangu, nakuwa sina cha
kusema, kubisha nashindwa, kumkufuru Mungu nashindwa, nabaki kuugua
moyoni kwa kiwango kisichotamkika.”
MATUSI YANAHUSU NINI HASA?
“Unakuta mtu amekualika
kwenye tamasha. Kwa bahati mbaya ama kwa kusahau ratiba au kuingiliana
majukumu, unaposhindwa kufika, inasambazwa kuwa umetapeli. Unapelekwa
polisi wakati mwingine nakuwa nimewasiliana na mhusika juu ya kutofika,
namuuliza nimrudishie pesa yake au kama ataandaa tamasha jingine
nihudhurie, unashangaa maneno ya utapeli yanaibuka,” alisema Rose.
KILIO CHAANZA!
Rose alishindwa kuhimili
kiwango cha maumivu ya moyo na kujikuta akiangua kilio hali
iliyomlazimu mwandishi kupata wakati mgumu kumtuliza.
“Oke, nikatukanwa kuwa
natumia unga. Ngoja nikuulize. Ingekuwa natumia unga, hivi kweli
ningeweza kutunga nyimbo, kuimba na kujituma kwa namna hiyo? Nakuuliza,
ninge.... (kilio kikubwa).
AKAENDELEA
“Niliowaamini ndiyo
wamenigeuka, wamenitumia kwa muda mrefu na wakati mwingine kwa
kunifanyisha kazi ambazo sikuwa nazitaka lakini wameona haitoshi, ni
haohao waliniteka na kunipeleka porini na kunitishia maisha. Mungu
atajibu na mbingu zitasimama (safari hii kwa kilio cha juu zaidi).”
ENDELEA NAYE
“Wengine wamekuwa
wakinitaka kimapenzi (akataja jina), lakini kwa kutumia pesa zao
nikikataa wananitishia maisha, wana wake na watoto, nabaki najiuliza
kwani mimi ni kafara ya waume za watu? Eeh? Kweli jamani? Nimepelekwa
porini, nikapigwa, nikaoneshwa mambo ya ajabu kweli, ili nitoe penzi kwa
nguvu, yote hayo nasingiziwa makubwa na kunenewa mabaya, nina moyo
wenye nyama, naumia.
“Nimewakosea nini
walimwengu? Tatizo ni kuimba? Hivi hawa Wakristo hawaoni kwamba nimekuwa
biashara yao nzuri kwa kuimba nyimbo nyingi zinazopendwa na wengi?
Hawalioni hata hilo? Nitende wema gani wa kupitiliza hapa?”
YOTE TISA, KUMI HII HAPA!
“Wameninyang’anya vitu
vyangu vingi ikiwemo vya ndani, viwanja, na wote ni waume za watu
walionitongoza na kuwakataa, wengine nilifanya nao kazi kwa ukaribu,
mfano... (akataja jina) na wametumia nafasi hiyo kunipokonya vitu hivyo
na wanajua kwa undani uhalali na umiliki wake. Hii ni haki kweli?
“Watu wanaposikia tu
Rose Muhando tapeli sasa waelewe napitia mateso magumu yanayoumiza mno,
wasisikie tu naimba hivi na kudhani nina furaha ya maisha, nateseka
nafsini! (kilio cha kwikwi).
AWEKA NUKTA
Katika kumalizia
mazungumzo na mwandishi wetu, Rose alisema: “Waniache na safari yangu ya
kumtumikia Mungu, ninachojua yeye (Mungu) atashughulika na watesi wangu
na kila nafsi itayaonja mauti.”
Risasi Jumamosi
linafanya juhudi za makusudi kuwasaka watu waliotajwa kwenye sauti ya
Rose ili kuwasomea madai yake.
#GPL
0 comments:
Post a Comment