Waombolezaji wakiwa
wamebeba jeneza lenye mwili wa Mhariri wa Kampuni ya Mwanahalisi, Edson
Kamukara wakati ulipowasili viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam jana
asubuhi, kwa ajili ya kuagwa. Kamukara alifariki dunia juzi na mazishi
yake yanatarajia kufanyika nyumbani kwao Muleba mkoani Kagera.
Mwenyekiti wa Umoja wa
Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Reginald Mengi
(katikati), akiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Dk.Wilibrod Slaa kwenye uagaji wa mwili wa Edson Kamukara.
Kulia ni Mbunge wa Bukoba mjini, Khamis Kagasheki.
Mmoja wa waandishi wa habari akiwa amepoteza fahamu wakati wa kuaga mwili huo.
Wanahabari na waombolezaji
wengine wakiwa wamejipanga foleni wakati wa utoaji wa heshima za mwisho
kwa mwili wa marehemu Edson Kamukara.
Mkurugenzi wa Kampuni ya
Mwanahalisi, Said Kubenea (katikati), akisaidiwa baada ya kuishiwa nguvu
wakati akitoa heshima za mwisho kwa marehemu.
Wanahabari ni huzuni na vilio.
Mwenyekiti wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akisalimiana na Mbunge
wa Bukoba mjini, Balozi Khamis Kagasheki wakati wa kuuaga mwili wa Edson
Kamukara.
Wanafamilia ya marehemu wakiwa kwenye shughuli hiyo.
Sehemu ya umati wa watu katika shughuli hiyo.
Mwakilishi wa wanafunzi
waliosoma na marehemu Shule ya Sekondari ya Majengo, Joachim Mushi
akizungumza kabla ya kutoa rambirambi yao ya sh.500,000.
Viongozi wa serikali na vyama vya siasa wakiwa kwenye shughuli hiyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.
Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni, Paul Makonda akizungumza katika uagaji wa mwili wa marehemu
ambapo alipigania waajiri wa vyombo vya habari kutoa mikataba ya ajira
kwa wanahabari.
Mwenyekiti wa Umoja wa
Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Regnald Mengi akimfariji
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea alikuwa akifanyakazi
marehemu Edson Kamukara.
Ni vilio tu kwa wanahabari.
Shughuli ya uagaji ikiendelea.
Dada ya marehemu Edson Kamukara akitoa heshima za mwisho.
#Habari za jamii.com
0 comments:
Post a Comment