Friday, May 8, 2015

CUF YATANGAZA WALIOPITA HATUA YA MWANZO KUGOMBEA UBUNGE NA UWAKILISHI ZANZIBAR

 Ofisa wa Uchaguzi wa CUF Ndg. Muhene Said Rashid, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar kuhusiana na Uteuzi wa Wagombea wa Ubunge na Uwakilishi katika majimbo ya Zanzibar hafla hiyo imefanyika wakati wa kutangaza majina hao iliofanyika katika Ofisi ya CUF Vuga.Kila Jimbo kimepitisha Wagombea Watu kupigiwa Kura na kwa Wananchi, ili kupatikana mgombea mmoja kushiriki Uchaguzi Mkuu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF Mhe Omar Ali Shehe akitangaza Majina ya Wagombea watatu kila Jimbo waliopendekezwa kugombea nafasi hizo na kuelezi jumla ya Wanachama wa CUF wamejitokeza kugombea nafasi hizo kwa Upande wa Ubunge waliojitokeza 517, Uwakilishi 212 na Viti Maalum Wanawake 67. Wanasubiri kupigiwa kura katika majimbo yao na wananchi ili kupatikana jina moja kuweza kushiriki katika uchaguzi Mkuu wa Zanzibar mwishoni mwa mwaka huu. 
Waandishi wakifuatilia hafla hiyo ya kutangazwa wanachama wa CUF waliofanikiwa kuingia hatua ya kwanza ya uchaguzi wa kugombea nafasi ya Ubunge na Uwawakilishi Zanzibar.



Baadhi ya Wanachama wa CUF waliojitokeza kugombea Nafasi za Uwakilishi na Ubunge wakifuatilia mkutano huo wa kutowa majina yaliopitishwa katika mchakato wa mwazo kuwapata wagombea na kupigiwa kura na wananchi kushiriki uchaguzi mkuu wa Zanzibar.,
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo wa kutangaza Majina ya Wanachama wa CUF waliopendekezwa kugombea Nafasi ya Ubunge na Uwawakilishi Zanzibar.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI