Pacquiao alikuwa mwenye furaha wakati akionyesha uwezo wake mbele ya umati uliojitokeza kwenye gym ya Wild Card
********
UKIMUULIZA Manny Pacquiao kwa nini anaamini ndondi ndiyo mchezo babu kubwa, hatakutajia dola za Kimarekani Milioni 120 na zaidi atakazolipwa kwa kuzichapa na Floyd Mayweather katika pambano la kihistoria Mei 2, mwaka huu mjini Las Vegas, Marekani.
Zaidi kumbukumbu zake zitarudi nyuma wakati PacMan alipokuwa PacKid, kijana mdogo wa miaka 12 katika viunga vya Ufilipino, wakati ambao mama yake alikuwa anatoka kwenda kutafuta chakula kila siku.
"Mtu fulani aliniambia mimi na rafiki zangu, kuna mapambano yanafanyika pale mjini,"alikumbushia. "Sikuwa najua ngumi ni nini wakati huo, lakini wakaniambia wanakupa zawadi kwa matokeo yoyote yale. Pesa mia mbili (dola mbili) kwa mshindi, mia kwa anayeshindwa.
Bondia huyo wa Ufilipino akifanya mazoezi chini ya kocha wake Roach
"Hivyo nilikwenda na nikashinda. NIkapeleka hizo dola mbili nyumbani na kumpa mama yangu, hivyo akaongeza chakula mezani. Lakini aliponiuliza nilipokuwa ninapata fedha, sikumuambia ni kwa ajili ya kupigana.
"Tulikuwa tunakwenda kila Jumapili na nikaendelea kushinda dola mbili. Kisha mjomba wangu akaniletea video za mapambano ya Ali, Foreman na Holyfield na wengine wengi,". Na hapo (ndondi) ikaanza,".
"Ngumi ni mchezo mzuri duniani, kwa sababu unakufundisha kuhusu maisha,"amesema. "Imenifundisha utapokea kama utarudisha,"anasema. Hilo ndilo ndilo somo analotaka kumpa Mayweather.
"Pambano hili likiisha, ningependa tukae chini kimya na tuzungumze,"anasema Pacquiao. "Nataka nizungumze naye kuhusu Neno la Mungu jinsi gani kila kitu tunachopata ni zawadi kutoka kwa Mungu. Kiasi gani tumebarikiwa kwa zawadi hizi na tunatakiwa kuzitumia kwa mambo mema,"amesema.
0 comments:
Post a Comment