WATU saba wamefariki dunia 26 wamejeruhiwa baada ya basi la Msanga Express likitokea Morogoro kwenda Mahenge kugongana na basi la kampuni ya Luwinzo lililokuwa likitoa Njombe kwenda jijini Dar es Saalam katika eneo la hifadhi ya Mikumi barabara ya Morogoro Iringa.Wananchi walioshuhudia tukio hilo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa basi la Msanga Express alikuwa akijaribu kulipita lori bila tahadhari na kisha kutoa gari barabarani wakati akikwepa ajali ya uso kwa uso ambapo aligongwa upande wa kulia.Inaelezwa kua watu sita walifariki dunia papo hapo na mwingine amefariki wakati akiwa njiani kupelekwa hospitalini kupata matibabu.Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amesema hadi sasa mwili mmoja tu ndiyo uliotambulika na miili mingine sita bado haijatambulika na imehifadhiwa katika hospitali ya St Kizito Mikumi.
Amesema madereva wa mabasi yote wamejeruhiwa na wanaendelea na matibabu wakiwa chini ya ulinzi ambapo kufuatia kuongezeka kwa mtukio ya ajali za mfululizo katika hifadhi ya Mikumi jeshi la polisi kwa kushirikiana na hifadhi ya Mikumi waanza kufanya oparesheni maalum kukagua madereva wanoendesha kwendo kasi katika hifadhi.
Katika hospitali ya St. Kizito walikolazwa majeruhi muuguzi wa zamu Josefu Masenga amekiri kupokea majeruhi 26 na kueleza amesema hali za majeruhi wanaendelea na matibabu huku majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa wakieleza jinsi tukio lilivyotokea.
#ITV
0 comments:
Post a Comment