Friday, February 13, 2015

USISHANGAE ENDAPO UTAPATA UJUMBE TOKA KWA MAREHEMU KUPITIA FACEBOOK, SOMA UJUE UNDANI!


MTANDAO wa kijamii Facebook umeongeza mazingira mapya ambayo yatampa mtumiaji wa mtandao huo uamuzi juu ya kurasa zao kuwa zifutike kabisa katika mtandao huo pindi watakapo fariki dunia.
Ama kama watataka kumchagua rafiki ama mwanafamilia atayeendelea na ukurasa huo na kudhibiti baadhi ya masuala katika ukurasa huo baada ya kifo chao.
Mazingira hayo ni moja ya madai waliyokuwa wakiyahitaji watumiaji wa mtandao huo wa kijamii ambao walitoa maoni yao juu ya ukurasa wa kumbukizi na taratibu zake.
Hata hivyo utaratibu huo mpya kwa kuanzia utaanza kutumika nchini Marekani.
Akitangaza utaratibu huo mpya ,mtandao huo wa kijamii umeeleza kuwa ,mtu akifa ukurasa wake unaweza kubaki kuwa kumbukumbu ya maisha yao hapa duniani,lakini pia ishara ya urafiki na uzoefu.
Kwa kuzungumza na watu waliopoteza wapendwa wao,tuligundua kuwa kuna kitu tunaweza kufanya kuwaunga mkono wale wanaoomboleza na wale wanaotaka kusema kitu kwenye kurasa za marehemu .
Kama mtumiaji ataamua kumruhusu mtu Fulani kuendeleza ukurasa wake hata katika siku ya mazishi na hatimaye maziko anaweza kufanya hivyo pia.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI