Thursday, February 19, 2015

CHUKUA HII MDADA: MADHARA YA KUCHORA TATTOO KIAFYA


TATTOO ni moja kati ya pambo kama mapambo mengine kama vile uvaaji hereni,cheni au kusuka.Wanawake huchora tattoo sehemu tofauti tofauti za mwili kutokana na mapenzi yake kwa mfano wengine hupenda kuchora shingoni,pajani,mkononi na kwabaadhi ya watu huthubutu kuchora hata katika sehemu zao za siri bila hata haya umeanika uchi wako kwa tattoo artist eti akuchore hapo sirini ,jamani watu wanahatari.
Kwa mdada wa kitanzania kwa hali ya kawaida kuchora tattoo sio jambo la kawaida sana kutokana na ukweli kwamba huu si utamaduni wetu bali ni utamaduni wan chi za kimagharibi kama vile Marekani,Uingereza na nyinginezo,ndio maana katika maeneo mengi hapa nchini kwetu ikitokea umemwona mdada amechora tattoo lazima utashtuka na kuna fikra hasi/mbaya zinakujia akilini juu ya tabia ya dada yule hata kama hunauhakika kama anatabia nzuri au mbaya, sijui kama hali hii imeshawahi kukutokea.
Uchoraji wa tattoo kwa mdada wa kitanzania si jambo la kujisifu wala si la kuona fahari eti utaonekana mjanja au mtu unayekwenda na wakati kwani katika jamii yetu hili si jambo lililozoeleka hivyo kwa kiasi kikubwa utakuwa unakutana na changamoto kadhaa achilia mbali matatizo ya kiafya ambayo unaweza kupata kama vile magonjwa ya kansa ya ngozi.
Miongoni mwa changamoto utakazokutana nazo ni kama vile kuhusishwa au kudhaniwa kuwa ni Muhuni na mtu mwenye tabia chafu ambaye hustahili kuigwa katika jamii.Watu watakuchukulia kama mtu uliyeshindikana hata kama katika hali halisi hauna hizo tabia kabisa,hivyo kama umejichora tattoo usije ukashangaa wanajamii wasipokupa ushirikiano wa kutosha katika baadhi ya mambo kwani unaonekana tofauti na wanajamii wengine wa kawaida.
Wanaume wenye maadili na hadhi ya kiafrika hakika hawatakuwa karibu na hata huwezi kumshawishi chochote kuingia katika uhusiano na mdada aliyejichorachora tattoo kwani huamini kuwa wewe ni muhuni na mchafu wa tabia,hivyo utapata changamoto kuolewa au kuwa katika uhusiano na watu wenye malengo ya kutengeneza familia badala yake utajikuta unaingia katika uhusiano na mwanaume mwenye akili za kimagharibi kama wewe ambaye si muoaji au mwenye tabia za ajabu ajabu ambao wamezoeleka kuitwa pasua kichwa.
Hivyo mdada wa kitanzania Urembo sio lazima ujichorechore tattoo kwani si sehemu ya utamaduni wetu,binti wa kiafrika hujitunza,hujithamini na kuheshimu watu wengine na ndio maana hata hao wazungu huwa wanawapenda sana wanawake hawa kuliko hata wazungu wenzao ambao wamejawa na tabia za ajabu ajabu zisizoweza hata kuvumilika na mzungu mwenzie 

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI