Saturday, January 24, 2015

RAIS KIKWETE AOMBOLEZA KIFO CHA MFALME ABDULLAH BIN ABDUL AZIZ AL SAUD WA SAUDI ARABIA

Saudi King Abdullah bin Abdulaziz Al Saud attends prayers on the first day of Eid al-Fitr which marks the end of the holy month of Ramadan, at Al-Safa Palace in Mecca August 30, 2011. REUTERS/Saudi Press Agency/Handout   (SAUDI ARABIA - Tags: POLITICS RELIGION ROYALS) FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS. THIS IMAGE HAS BEEN SUPPLIED BY A THIRD PARTY. IT IS DISTRIBUTED, EXACTLY AS RECEIVED BY REUTERS, AS A SERVICE TO CLIENTS
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameituma Saudi Arabia salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha
Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud (90) ambaye alifariki, Alhamisi, Januari 22, 2015, na kuzikwa jana, Ijumaa, Januari 23, 2015 mjini Riyadh.
Katika salamu zake kwa Mfalme mpya, Mfalme Salman bin Abdul Aziz al Saud, Rais Kikwete amesema kuwa anaungana na wananchi wa Saudi Arabia na dunia nzima kuomboleza kifo cha kiongozi aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Saudi Arabia na katika siasa za eneo la Mashariki ya Kati kwa jumla na kwa muda mrefu.
Ameongeza Rais Kikwete: “Katika miaka yote 10 ya utawala wake tokea 2005 na kabla ya hapo katika miaka mingine 10 wakati anashikilia utawala badala ya kaka yake Mfalme Fahd aliyekuwa anaumwa, Mfalme Abdullah alithibitisha uongozi wa kuwajibika na msimamo thabiti wa kutafuta amani katika Mashariki ya Kati na dunia itaendelea kumkumbuka kwa mchango huo.”
Amesisitiza Mhe. Rais Kikwete:  “Aidha, sisi katika Tanzania tutaendelea kuenzi juhudi zake kubwa za kujenga na kuimarisha uhusiano wa karibu kati ya nchi zetu,” amesema Rais Kikwete.
“Kwa niaba ya wananchi wa Tanzania, Serikali ninayoiongoza na mimi mwenyewe, nakutumia wewe Mfalme Salman salamu za rambirambi, na kupitia kwako kwa wananchi wote wa Saudi Arabia kwa kuondokewa na kiongozi wao.  Sisi katika Tanzania tunaungana nanyi kuomboleza na kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke peponi roho ya Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud. Amen.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
23 Januari,2015

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI