Thursday, January 1, 2015

MAUAJI..!! MFUGAJI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA ASKARI HUKO SIMIYU

Mfugaji jamii ya Kitaturu alivyokutwa amekufa baada ya kupigwa risasi na askari wa wanayamapori wa kampuni ya uwindaji ya MWIBA katika eneo tengefu la Maswa huko wilayani Meatu Mkoani Simiyu.
******
JESHI la polisi mkoani Simiyu linawashikiria watu 4 askari wa wanayapori katika eneo la hifadhi ya wanyama ndani ya eneo tengefu la Maswa (Maswa game Reserve) Wilayani Meatu kwa kosa la kumpiga risasi mfugaji hadi kusababisha kifo chake.
Askari hao ambao wanafanya kazi katika kampuni ya Mwiba inayojihusisha na uwindaji ndani ya eneo hilo, walimpiga risasi mfugaji huyo baada ya kutokea mapigano makubwa baina yao na wafugaji waliokuwa wakichunga ng’ombe ndani ya eneo hilo.
Akitoa taarifa ya tukio hilo mbele za waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Charles Mkumbo alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 7:00 mchana katika kata ya Mwangudo wilayani humo.
Mkumbo alieleza kuwa askari hao wakiwa kazini eneo la Mayoyi ndani ya hifadhi hiyo walimkamata Giganga Sinyau (40) mfugaji pamoja na ndugu yake Matofari Sinyau wote wakazi wa kijiji cha Lukale wakichunga ngo’mbe wao ndani ya eneo hilo kinyume cha sheria.
Alieleza kuwa baada ya wafugaji hao pamoja mifugo yao kukamatwa walipiga yowe ambapo kundi kubwa la wafugaji kabila la wataturu, ambapo Mkumbo alieleza kuwa walikuwa wakichunga mifugo yao katika eneo jingine.
Alisema baada ya kundi hilo kufika walipokuwa wamekatwa wafugaji wenzao walianza kurusha mishale, ambapo askari mmoja wa wanayamapori Dotto Makanga (24) alijeruhiwa kwa mshale katika paja la mguu wake wa kulia.
“..katika kujihami askari hao walianza kupiga risasi hewani na nyingine kuwashambulia wafugaji hao….katika kurishiana huko Giganga Sinyau alipigwa risasi katika paja la mguu wake wa kulia kisha kudondoka chini” Alisema Mkumbo.
Aidha kamanda Mkumbo alibainisha kuwa mfugaji huyo baada ya kupigwa risasi aliweza kutokwa na damu nyingi bila ya kupewa msaada wowote hadi kupoteza uhai wake, huku akibainisha kuwa wafugaji hao walikuwa wameengiza zaidi ya ngo’mbe 2000 ndani ya eneo hilo.
Aliwataja askari hao wanaoshikiliwa na jeshi la polisi Meatu kuwa ni Reonald Rukasi (30), Mboje Donald (29), Sanka Simon (38) pamoja na Kichelula Malashia (40), huku akibainisha kuwa wanawashikiri kwa ajili ya uchunguzi zaidi kama walitumia nguvu kubwa katika kujiami.
Hata hivyo Mweneyekiti wa wafugaji kanda ya ziwa Mulida Mushota akizungumzia tukio hilo mbele za waandishi wa habari alisema kuwa taarifa ya jeshi la polisi siyo kweli.
Mulida alibainisha kuwa mfugaji huyo alikuwa akiamisha mifugo yake kwenda sehemu nyingine kwa ajili ya kutafuta malisho, na kubainisha kuwa askari wa kampuni hiyo ya uwindaji ndani ya eneo hilo (Mwiba) walimkamata na kuanzi kumpiga hadi kumsababishia kifo chake.
“…ukweli wa tukio ni kwamba huyu mfugaji baada ya kukamatwa na mifugo yake ambayo haikuwa ndani ya hifadhi….alianza kujiami na alipowazidi nguvu askari hao wote walipiga risasi hadi kusababisha kifo chake papo hapo” Alisema Mulida.

Alibainisha taarifa ya jeshi la polisi inalinda kampuni hiyo, na kubainisha kuwa hayakuwepo mapigano kama inavyodaiwa na jeshi hilo wala wafugaji wengi walikuwa wakichunga ngo’mbe ndani ya eneo hilo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI