WATU 20 wamepoteza maisha huko Afghanistan wakati wa Sherehe za Harusi baada ya kutokea kwa mashambulizi ya Rocket.
Zaidi ya watu 40 wamejeruhiwa wakati Rocket ilipodondokea katika moja ya nyumba ambazo hutumika kwaajili ya maharusi kaskazini mwa jimbo la Helmand,wengi wa waliopoteza maisha ni wanawake na watoto.
Watu Waliojeruhiwa katika tukio hilo walipelekwa eneo la jimbo kuu katika hospitali ya Lashkar Gah.
Tukio hilo limetokea disemba 31 wakati wa mapigano kati ya wanajeshi wa Afghanstan na wanamgambo wa Taliban ikiwa ni Siku ya mwisho wa mpango wa majeshi ya marekani na Nato nchini humo.
Mwaka 2014 umekuwa ni mwaka wa umwagaji damu nchini Afghanistan ambapo zaidi ya wanachama wa vikosi vya usalama 4600 walipoteza maisha katika mapigano dhidi ya Taliban.
Kwa upande wa vikosi vya kigeni askari 3500 wamepoteza maisha tangu kuanza kwa mpigano na vikosi vya kujihami vya umoja wa mataifa NATO.
LIKE PAGE YETU KUFUATILIA MATUKIO ZAIDI.
LIKE PAGE YETU KUFUATILIA MATUKIO ZAIDI.
0 comments:
Post a Comment