KLABU ya Manchester City imethibitisha kuwa Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza Frank Lampard ataendelea kubakia katika kikosi hicho mpaka mwishoni mwa msimu huu.
Lampard alijiunga na Klabu ya Manchester City kwa mkopo kwa muda wa miezi sita akitokea katika klabu ya New York City Red Bulls ya Marekani baada ya kuondoka Chelsea mwishoni mwa msimu uliopita.
Taarifa rasmi iliyotolewa na klabu hiyo Manchester City imethibitisha kuwa imemwongezea mkataba Frank Lampard huku ikifafanua kuwa ataruhusiwa kushiriki mashindano ya Ligi kuu pamoja na Mashindano ya ngazi ya vilabu yatayoihusu klabu hiyo.
Lampard 36 amefunga jumla ya magoli sita msimu huu tangu kuanza kuitumikia klabu ya Manchester City.
LIKE PAGE YETU KUFUATILIA MATUKIO ZAIDI.
LIKE PAGE YETU KUFUATILIA MATUKIO ZAIDI.
0 comments:
Post a Comment