Sunday, December 21, 2014

WAKAZI WA MTAA WA MIGOMBANI WAGOMEA KURUDIA UCHAGUZI WA NAFASI YA MWENYEKITI WA MTAA WA MIGOMBANI KATA YA SEGEREA

Wakazi wa Mtaa wa Migombani wakimzonga Afisa Mtendaji wa Kata ya Segerea ambae amekuja kutangaza kurudia uchaguzi wa Nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Migombani leo ambao ulifanyika tarehe 14 Disemba 2014 ambapo mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti Japhet Kembo Kutoka Chadema aliibuka  Mshindi kwa Kura 547. Wakazi hao wamegoma kurudia uchaguzi huo kutokana na kile ambacho Afisa Mtendaji huyo alitangaza katika uchaguzi wa Mtaa huo uliofanyika tarehe 14 Disemba 2014 kuwa Uchaguzi ni Halali na Matokeo pia yatakuwa halali.
Hii ndio barua iliyoandikwa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Segerea kutangaza kuwa uchaguzi wa Serikali ya Mtaa wa Migombani uliofanyika tarehe 14 Disemba 2014 ikieleza kuwa Uchaguzi ni halali na Matokeo yatakuwa halali
Wakazi wa Mtaa wa migombani wakigomea kurudiwa uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Migombani
 Afisa Mtendaji wa Kata ya segerea(anayeongea na simu) akiongea na simu na anayesemekana kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Manispaa ya Ilala ambae anamuhamrisha Kutangaza kurudia Uchaguzi wa Nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Migombani Ilihali Uchaguzi huo uliofanyika tarehe 14 Disemba 2014 ulikuwa wa amani na haki.
Wakazi wakigomea kurudiwa kwa uchaguzi wa Nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa..
Picha Zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI