Monday, December 8, 2014

TV 1 TANZANIA YAWA KIVUTIO KIKUBWA KATIKA TAMASHA LA NYAMA CHOMA FESTIVAL GRAND FINALE 2014 *PICHAZ*

Banda la TV 1 Tanzania katika tamasha la Nyama Choma Festival Grand Finale 2014. 
MAANDALIZI…!

Baadhi ya wachoma nyama wakiendelea na maandalizi katika tamasha la Nyama Choma Festival Grand Finale 2014.
Team ya TV 1 Tanzania #Edgar Wilson #Geofrey, #Wambura Mapenda wakiendelea na maandalizi katika tamasha la Nyama Choma Festival Grand Finale 2014.

Na Frank Mavura, Dar es salaam
TAMASHA la Nyama Choma ni tamasha ambalo limejizolea umaarufu mkubwa kwa miaka ya hivi karibuni tangu kuanzishwa kwake jijini Dar es salaam na kusambaa katika maeneo mengi ya jiji hatimaye katika mikoa kadhaa nchini.
Udhamini ni kitu cha muhimu sana ili kufanikiwa kwa tamasha hili, kitu ambacho Kituo bora cha Burudani nchini Tanzania cha TV 1 kimefanikisha hilo kwa kuamua kuwapa burudani zaidi watazamaji wake kwa kuhakikisha uchomaji na ulaji wa nyama pamoja na burudani mbalimbali za miziki unafanikiwa.

Afisa Mahusiano wa TV 1 Tanzania Bw. Mponjoli Katule.
Akiongea kwa njia ya simu na mwandishi wa mtandao huu wa Ulimwengu wa habari Bw. Mponjoli Katule ambaye ni Afisa mahusiano wa TV 1 Tanzania ameongelea furaha waliyonayo kama kituo cha Televisheni kushiriki katika utoaji wa burudani kwa wananchi wengi waliojitokeza katika Tamasha la Nyama choma Festival, Grand Finale lililofanyika tar 06/12/2014 katika viwanja vya michezo vya Chuo kikuu cha Dar es salaam;
"Tunajisikia vizuri sana kuwa sehemu ya watu waliochangia kutoa burudani kwa wananchi kwasababu hiyo imekuwa ni moja ya kitu tunachokipa mkazo zaidi".

Afisa Mahusiano wa TV 1 Tanzania Bw. Mponjoli Katule akimkabidhi T-Shirt Muandaaji wa Tamasha la Nyama Choma, Bi. Carol Ndosi katika tamasha la Nyama Choma Festival Grand Finale 2014.
Bw. Katule ameongeza kuwa kama kituo cha burudani ni wajibu wao kuwaburudisha watazamaji wao;
"Kama ilivyo kauli mbiu yetu TV 1 Tanzania ni Kituo bora cha burudani hivyo tunawaomba watazamaji wetu waendelee kuiangalia TV yetu ili wapate kuburudika lakini pia kuelimika kupitia vipindi bora vinavyorushwa na TV yetu, kama vile: 'The one show', 'Boys Boys', 'Habari', 'The Parkage' na vingine vingi ambapo tunapatika kupitia king'amuzi cha Startimes".
Wadau mbalimbali walojitokeza katika tamasha hilo wakila Nyama Choma.
 Wadau mbalimbali walojitokeza katika tamasha hilo wakila Nyama Choma.
Wageni nao walojitokeza katika tamasha hilo na kula Nyama Choma.
Licha ya watu mbalimbali kukusanyika kwa lengo la kula nyama na kufurahi, Tamasha hili huwapa fursa zaidi wafanyabiashara kuuza vyakula ambapo baadhi wanasema kuwa nyama na vinywaji hupata soko zaidi ambapo pia hupata fursa ya kuonja nyama katika mabanda mengine mbalimbali hivyo kupata uzoefu mpya wa namna bora zaidi ya kuchoma nyama.
Tamasha hilo huwavuta baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam kutokana na ubora unaoambatana na ushindani katika uchomaji nyama hivyo kupata nyama choma yenye ladha nzuri na iliyochomwa vizuri.
WACHEZA SAMBA SASA..!
Mwaka huu waandaaji wa Tamasha hilo wameongeza burudani zaidi kwa kuwaalika watoa burudani toka Brazil na kufanya yao 'Samba Parade'

Wacheza Samba wakifanya yao na mashabiki lukuki wakionekana kuvutiwa na Parade hii iliyofanyika katika tamasha la Nyama Choma Grand Finale 2014.

Samba inaendeleaaa….!

Wadau wakiendelea kufuatilia Samba Parade!

Tamasha la nyama Choma lilianza rasmi mwaka 2001 ambapo hufanyika mara nne kwa mwaka na kuzunguka katika baadhi ya mikoa kama Dodoma, Mwanza na Mbeya.
Haya sasa Wafanyabiashara wa Nyama choma na vinywaji tumieni fursa za Matamasha mbalimbali yanayojitokeza nchini kwa lengo la kuuza biashara zenu kwa wingi ikiwa ni pamoja na kujitangaza kibiashara sambamba na kupata ujuzi wa namna watu wengine wanavyochoma nyama ili kuwavutia wateja zaidi mnaporudi katika maeneo yenu ya kazi.
Wafanyakazi wa TV 1 Tanzania nao walijitokeza katika tamasha hilo la Nyama Choma Festival Grand Finale 2014.

Bw. Silas Lameck akiwa katika pozi.

Bw. Ibrahimu Matukuta akila nyama choma.

Bw. Geofrey akiwa katika pozi.

FANS WA TV 1 TANZANIA..!

Baadhi ya mashabiki wa TV 1 Tanzania wakitokelezea katika mapozi tofauti huku Tamasha la Nyama choma likiendelea.

Mashabiki wa TV 1 Tanzania ambao walijitokeza katika banda la TV 1 kwaajili ya kupata maelekezo mengi juu ya uendeshaji wa vipindi na kupiga picha mbele ya bunners za TV 1 ambapo wengi wameipa sifa runinga hiyo kuwa kweli ni kituo bora cha Burudani Tanzania.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI