Sunday, December 14, 2014

ANGALIA JINSI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA ULIVYOKWENDA SIKU YA LEO

 MAENEO mengi ya jiji la Dar es salaam hii leo wamefanya uchaguzi wa Serikali za Mtaa ambapo wananchi wengi waliojitokeza wamejitokeza kutumia haki yao ya msingi ya kidemokrasia ya kupiga kura. Picha mbalimbali zikionesha watu wakishiriki katika zoezi hilo licha ya kasoro chache zilizojitokeza kwa baadhi ya maeneo ambapo baadhi ya maeneo wameahirisha uchaguzi huo kutokana na kukosekan kwa karatasi za kupigia kura huku baadhi ya maeneo majina ya wapiga kura yakiwa hayana nembo stahili ya mgombea mfano mgombea wa Chadema akawekewa nembo ya CUF.
 Mkazi wa Kipunguni B, Onesphory Mrina akipiga kura yake.
 Baadhi ya vituo kam ahiki amani ilitawala hapa ni Kipunguni B huko Moshi Bar kata ya Kivule Wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam.
 Wakazi wa Mazizini wakihakiki majina yao.
 Wakazi wa mazizini Ukonga wakisubiri kuingia kupiga kura.
 Mkazi wa Mazizini Ukonga, Gerald Mugumira akionesha kidole chake baada ya kupiga kura yake ya kuwachagua viongozi wao.
 Wakazi wa Mtaa wa Kilimahewa Wilaya ya Temeke , wakipiga kura
Wakazi wa Kilimahewa huko Temeke wakisubiri kupiga kura.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI