Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred akiwa katika picha ya pamoja na walemavu wa ngozi mara baada ya kumaliza mafunzo ya usajisiriamali kwenye viwanja vya Makumbusho ya Taifa jijini.
Na Mwandishi wetu
Taasisi ya Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred Foundation (BAF) imeendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana 50 wenye ulemavu wa ngozi.
Brigitte aliendesha mafunzo hayo kwa kushirikiana na taasisi ya Junior Achievement Tanzania yalifungwa jana kwenye viwanja vya Makumbusho ya Taifa na kupambwa na maonyesho ya bidhaa za wajasiriamali mbalimbali ambao ni zao la mradi huo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Brigitte alisema kuwa mafunzo hayo yamelenga mambo mbalimbali katika maisha ya kila siku ikiwa pamoja na kuwawezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha ya kila siku.
Alisema kuwa BAF kupitia Taasisi ya Junior Achievement Tanzania kwa pamoja wameweza kutoa elimu ya kujitambua na stadi za biashara ili walemavu wa ngozi waweze kuthubutu, kuanzisha na kuendeleza biashara na shughuli nyingine za kiuchumi zitakazo wapa ajira, kipato na kuinua ustawi wa maisha yao na familia zao.
Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred akiteta na wanafunzi waliofika kuangalia jinsi mafunzo ya Ujasiriamali yakiendeshwa na Taasisi ya mrwembo huyo (BAF) na Taasisi ya Junior Achievements Tanzania.
Alisema kuwa mpango huu umekuwa wa kipekee kwa kundi hili kwa kuweza kuwajengea mtazamo chanya wakuthubutu, kujiamini na kuweza kufanya mambo makubwa katika maisha.
“Mpango huu umeanza hapa Dar es Salaam, ila Brigitte Alfred Foundation ina azma ya kuuendeleza nje ya Dar es Salaam na kufikia walengwa waliopo mikoa tofauti nchini kwa sababu umeleta manufaa na mabadiliko makubwa sana kwa hawa vijana wenye ulemavu wa ngozi katika muda mdogo na umeonyesha kwamba walemavu wakiwezewshwa,” alisema Brigitte.
Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred akiwa katika pozi na wanafunzi waliofika kuangalia jinsi mafunzo ya Ujasiriamali yakiendeshwa na Taasisi ya mrwembo huyo (BAF) na Taasisi ya Junior Achievements Tanzania.
Mrembo huyo alitoa shukrani kwa Juniour Achievement Tanzania na wadhamini wakuu, kampuni ya Azam kwa kutoa mafunzo hayo ambayo anaamini wahitimu watayatumia kwa faida zaidi.
“Nawaomba wadau wengine waniunge mkono katika mpango huu kwani awamu inayofuata ambayo ni kutekeleza mipango yao ya biashara katika ujasiriamali ili kuendeleza vijana wetu wa Tanzania hususa walemavu ili weweze kujikimu na kuboresha maisha yao kwa ujumla,” alisema.
0 comments:
Post a Comment