MKURUGENZI wa Idara ya Kinga kutoka taasisi ya Saratani Ocean road Julius Shija amewataka watanzania waache tabia ya kuiga mambo yasiyo ya msingi kama kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo tendo ambalo amelitaja kuwa linaweza kusababisha kansa ya koo.
Shija alisema kwamba hali katika kipindi cha hivi karibuni imebadilika kulinganisha na kipindi cha miaka ya tisini ambapo walikuwa wanapokea wagonjwa 200 hadi 300 tofauti na kipindi cha sasa ambacho wanapokea wagonjwa 500 hadi 600 ambao wanagundulika kuathiriwa na kansa iliyosababishwa na ufanyaji mapenzi kwa kuhusisha midomo.
"Watanzania wasipende kuiga mambo ambayo si sahihi bila kujua madhara yake kama kufanya mapenzi kwa kuhusisha mdomo, saratani ya mdomo ipo na nyingine zinasababishwa na zinaa," alisema Shija.
Aliongeza kuwa wanapokea wagonjwa wapya kila siku kwenye taasisi hiyo wagonjwa waliopata saratani hiyo mdomoni na kwenye njia ya juu ya hewa baada ya kujamiiana kwa njia ya mdomo.
"Kufanya mapenzi na kuhusisha mdomo kunaleta saratani kupitia mdomo na sehemu ya juu ya hewa, virusi hivi vikifika kwenye sehemu ya juu ya hewa na mdomoni na vikakuta kuna mchubuko au uwazi wowote vitaingia kwenye hizi chembechembe za fizi kwenye ulimi na kwenye njia ya juu yahewa, vitapenya ndani na kuharibu zile chembechembe na zitaanza kukua na kusababisha saratani," alieleza Shija.
0 comments:
Post a Comment