Jana
ndio Waziri mkuu mpya wa Uganda Ruhakana Rugunda kaapishwa ila kabla
yake alikua ni Amama Mbabazi ambae alifutwa kazi wiki kadhaa zilizopita
baada ya kukaa madarakani toka May 2011 akitokea kwenye Uwaziri wa
Ulinzi.September 18 2014 ndio Rais Museveni alimuandikia Spika wa bunge
barua kumuarifu kuwa ameamua kumuondoa waziri mkuu huyo na nafasi yake
kuchukuliwa na aliyekua Waziri wa Afya ambae kwa sasa ana umri wa miaka
67.
Kwa mujibu wa ripota wa TZA (millardayo.com
na AyoTV) waziri huyu alietimuliwa alikua Waziri mkuu wa nne toka Rais
Museveni aanze kuitawala nchi hiyo January 1986 ambapo mpaka sasa
amewahi kuwa na Makamu wa Rais wanaofikia wanne.
Picha
zote hizi zinaonyesha wakati Serikali ya Uganda ilipomnyang’anya ulinzi
wa Wanajeshi waziri huyu mkuu baada ya kufutwa kazi ambapo kwenye hii
picha ya chini anaeonekana ni mke wake akilalamika kwa kutoamini
kilichotokea kwani mume wake na Rais Museveni wamekua marafiki wakubwa.
Vyombo
mbalimbali vya habari vimeripoti kwamba kuna mambo mengi yaliyosababisha
kufutwa kazi kwa waziri huyu mkuu lakini mambo hayo hayajawekwa wazi.
Nyuma hii unayoiona ni nyumba anayoishi na inayomilikiwa na Waziri huyu mkuu aliefutwa kazi.
0 comments:
Post a Comment