MADEE alikamatwa na Polisi saa kadhaa zilizopita baada ya tukio la yeye kuibiwa simu akiwa kwenye gari tena likitembea ambapo waliohusika ni watu wawili wakiwa kwenye pikipiki saa tisa usiku akitoka Kigamboni Dar es alaam kufanya show hivyo akawa anavuka bahari ili aelekee nyumbani.
Baada ya kuchoropoa hiyo simu jamaa wa pikipiki walianza kukimbia hivyo na dereva wa Madee akaanza kukimbizana nao na kufanikiwa kuwagonga alafu pikipiki ikaanguka ila jamaa wa nyuma aliechoropoa simu akafanikiwa kukimbia ila yule aliekua anaendesha wakambeba na kwenda nae maskani Tiptop kwa lengo la kumuhoji ili wampate aliekimbia na simu.
Madee alipofatwa na kukamatwa na Polisi mtaani kuhusu hii kesi, aliandikwa kwenye page yake ya insta ‘hivi niliua au niliibiwa simu?’
(Picha: GP)
Kilichomfanya Madee akamatwe na kuwekwa Polisi ni madai yake kwamba kesi hiyo imegeuzwa na sasa yeye ndio anaonekana mwenye makosa kwa kumteka huyu jamaa waliekwenda nae Tiptop Manzese.
Haya ndio mambo 10 anayoyasema Madee.
1. Nilikaa Polisi kwa zaidi ya saa 32, nililala na kuamkia huko.
2. Kule ndani haupo huru ndio maana kuna mateso, unapangiwa muda wa kulala na hautakiwi kuongea kwa sauti kubwa… mle ndani watu wanatolewa njee saa moja usiku tunahesabiwa pale nje alafu mkishaingizwa ndani kimyaaaa.
3. Kwenye room niliyoshikiliwa nilikua na watu kama 30 hivi ila sijui kwenye room nyigine ya pili sijui kulikua na watu wangapi sababu sikuingia.
4. Nilianza kushangiliwa nilipotokeza tu pale kwa juu wakati naingizwa machizi waliponiona mimi wakaanza kuimba ule wimbo wangu wa ‘majuto ni mjukuu‘ niliozungumzia ishu za Polisi.
5. Nilivyofika kule nilikuta kumejaa ila kumbe kuna sehemu tayari nilishawekewa na machizi sehemu poa tu upepo unaingia fresh tu sema ndio hivyo mazoea mazoea tu huwezi kulala….
Madee aliipiga na kuiweka instagram muda mfupi baada ya kuachiwa kwa dhamana na kuandika ‘Am Freeeeeee’ akimaanisha yuko huru
6. Mle ndani hakuna vitanda zaidi ya sakafu tu nilitamani hata nijaribu kupeleka maombi niwapelekee machizi mikeka kidogo wawe wanalalia.
7. Nilisimamishwa Mahakamani September 25 kwa mara ya kwanza sababu jamaa wamejaribu kutengeneza vitu vingine viwili tofauti na ilivyokua, wanasema mimi nimemteka mtu na pikipiki yake nikaenda kumjeruhi na washkaji zangu ila ukweli ni kwamba huyu jamaa alikua na rafiki yake kwenye pikipiki wakanipora simu yangu wakati nikiwa nimekaa kwenye gari.
8. Baada ya hapo dereva wangu mtundu akakimbia akaiblock pikipiki na kuigonga wakaanguka lakini yule aliekua amechukua simu akakimbia ila aliekua anaendesha tukamkamata tukampakiza kwenye gari na kuondoka nae mpaka maskani ya Tiptop ila nikampigia simu mama yake nikamwambia mwanao yuko hapa njoo uongee nae aturudishie simu yetu.
9. Mama yake alikuja akaondoka na kusema anakwenda kumtafuta aliechukua simu lakini cha kushangaza Mama asubuhi akaja na Polisi wakamchukua jamaa na kumpeleka Magomeni wakati huo mi nilikua nimekwenda Mwanza kwenye show.
10. Niliporudi kutoka Mwanza nikakimbilia Polisi Magomeni kwenda kuulizia napataje haki yangu nikaambiwa hili shauri linahamishiwa Kigamboni, nilipokwenda Kigamboni Polisi nikakuta hiyo kesi kwamba Madee kamteka mtu nikawekwa ndani, hii ni kama mara yangu ya nne au ya tatu nawekwa Polisi…. hizo nyingine zilishatokea zamani ambapo ya mwisho ilikua miaka sita au saba nyuma, hii kesi ya sasa ipo Mahakamani.
0 comments:
Post a Comment