Amerudi kazini: Rojo akiwasili katika hoteli anayoshi mjini Manchester baada ya kuwa na timu ya taifa ya Argentina.
******
BEKI mpya wa Manchester United, Marcos Rojo amerejea kutoka kwenye majukumu ya taifa lake, Argentina kujiandaa kuanza kuichezea klabu yake hiyo mpya dhidi ya QPR Jumapili. Rojo bado hajaichezea klabu yake hiyo mpya licha ya kusajiliwa wiki tatu zilizopita kutokana na kuchelewa kupata hati ya kufanyia kazi England. Aliiwakilisha nchi yake kwenye Kombe la Dunia na akacheza kwa dakika zote 90 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ujerumani, Argentina ikilipa kisasi cha kufungwa kwenye fainali ya Kombe la Dunia.
Muargentina huyo anatarajiwa kuanza kuichezea United Jumapili katika Ligi Kuu ya England, baada ya suala lake la hati ya kufanyia kazi kupatiwa ufumbuzi.
Ujio wa beki huyo ni faraja kwa Louis Van Gaal, ambaye timu yake ilionekana kuwa na tatizo katika safu ya ulinzi, kiasi cha kufanya vibaya kwenye mechi za mwanzoni.
Safu ya ulinzi ya Mashetani hao Wekundu imeyumba baada ya kuondoka kwa mabeki wote wakongwe mwishoni mwa msimu, Patrice Evra, Nemanja Vidic na Rio Ferdinand.
0 comments:
Post a Comment